header

nmb

nmb

Saturday, August 28, 2010

WAFANYAKAZI TANESCO WATAKIWA KUNUNUA UMEME KAMA WATEJA WENGINE!!

NA MAGRETH KINABO

27/08/2010

BARAZA la Ushauri la Watumiaji Huduma zinazothibitiwa na NAMAGRETH KINABO NA ZAHRA MAJID- MAELEZO

27/08/2010

BARAZA la Ushauri la Watumiaji Huduma zinazothibitiwa na Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) limelishauri Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liondoe bei za viwango maalum vya umeme kwa wafanyakazi wake na wajumbe wa bodi ya shirika hilo kutoka T6 hadi T1 kama ilivyo kwa watumiaji wegine.

Hayo yalisemwa jana na Makamu Mwenyekiti wa EWURA CCC, Said Abeid wakati akitoa maoni juu ya ombi la TANESCO kuongeza bei ya umeme kwa awamu ambapo limeomba ongezeko la asilimia 34.6 kuanzia Januari 2011, asilimia 13.8 mwaka 2012 na asilimia 13.9 mwaka 2013 kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa viwango hivyo sh. 4.50 kwa uniti zisizozidi 750 kwa mwezi na viwango vya T1 kwa matumizi yanayozidi uniti hizo.

“Kama wafanyakazi wote 5,538 watatumia uniti zote, jumla ya matumizi hayo kwa mwezi yatafikia uniti 4.154 milioni kwa mwezi au uniti 49,842 milioni kwa mwaka. Haya ni matumizi makubwa yanayokaribia kulingana na matumizi ya mkoa mzima wa Kagera kwa mwaka 2010.

Akinukuu maelezo ya mtaalamu mwelekezi wa aliyeteuliwa na TANESCO kuchambua gharama na kuandaa bei ya huduma, ambaye ripoti inadokeza kuwa si sahihi kwa matumizi ya kundi kubwa la watumiaji wa huduma kufidiwa na makundi mengine.

Abeid aliongeza kampuni mbili za kigeni zizoteuliwa na TANESCO kwa ajili ya kutoa ushauri elekezi kuhusu gharama na maombi ya kuongeza bei yawe huru na si yakuajiriwa na shirika hilo ili kuepuka kuipendelea.

Hata hivyo Abeid aliongeza kwamba kuna tozo nyingi ambazo watumiaji wa umeme wanatozwa mfano gharama za kisheria kama 18% VAT , 3% REA na 1% ya EWURA, wasiwasi wa baraza hilo ikiwa bei zitapanda kama TANESCO inavyotaka huenda watu wengi wakashindwa kumudu huduma hiyo na idadi ya watumaji kupungua, hali itakayochangia bei ya nishati hiyo kuzidi kupanda.

Awali akitoa maelezo kuhusu ombi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando alisema shirika linapata hasara ya sh.41 kwa kila uniti inayouza kulingana na ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2008, hivyo kwa mwaka huo ilipata hasara y a sh. bilioni 21.6 kwa sababu makusanyo hayatoshelezi gharama za uendeshaji.

Alisema wastani wa gharama za kuuzia umeme ni sh.111 kwa uniti wakati za kumfikishia mteja ni sh. 152 kwa uniti.

Baadhi ya wadau wengine ambao, ni Janeth Muro na Ramadhani Shebe ambao walipinga hoja hiyo, waliitaka shirika hilo lidhibti tatizo la upotevu wa umeme linalodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wakishirikiana na wateja ambao si waaminifu.

Naye Kamishna Msaidizi wa Baraza la Ushauri la Serikali(GCC), Theophilo Bwakea alishauri kuwa TANESCO ielekeze nguvu za udhibiti wa upotevu wa umeme hasa kwa wateja wakubwa kuboresha huduma na kuongeza idadi ya wateja kutoka 100,000 mwaka mwaka kwa kuwa ni kidogo.

Maoni mengine TANESCO ichukue hatua za haraka za kupunguza matumizi yake yasiyo ya lazima kama vile gharama za utawala ambazo zinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka kwa kasi bila ya kuongeza tija ndani ya Shirika.

Pia tathimini ya mapato na matumizi ya Shirika kwa miaka ya nyuma na na mtiririko wake kipindi kifupi cha mbele inabainisha matumizi yanazidi mapato.

Baraza linashauri Shirika liongeze wigo wa wateja wakubwa, wa kati na wadogo ili liweze kusanya mapato mengi na kupunguza gharama za uendeshaji kwa kila mteja. Kuimarisha ufanisi katika ngazi zote za utendaji hakuepukiki ikiwa Shirika linataka kubaki kama mshindani wa kweli katika soko la biashara ya umeme nchini na katika nchi za Kikanda.

Akijibu hoja hizo Mhando alisema watazifanyia kazi changamoto hizo ili kuboresha huduma na ikiwemo kudhibiti upotevu wa umeme ambapo wameshaanza kuchuaka hatua kwa baadhi ya wahusika.

Mkurugenzi wa EWURA, Haruna Masebu alisema kuwa bado wadau wana nafasi ya kutoa mapendekezo kwa maandishi hadi Septemba 10 saa kumi na moja jioni.

No comments:

Post a Comment