header

nmb

nmb

Friday, August 27, 2010

WABUNIFU WA MITINDO NCHINI KUFAIDIKA NA MAFUNZO!!

Swahili Fashion Week kwa kushirikiana na Tanzania Cotton Board (TCB) na Textile Sector Development Unit (TSDU) kwa pamoja wameandaa mafunzo kwa wabunifu wa Tanzania yenye lengo la kuboresha taaluma ya ubunifu hapa nchini.

“Tunaamini kwamba baada ya mafunzo haya, wabunifu wa watanzania wataweza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zitaweza kuuzwa sehemu yoyote. Pia kupitia mafunzo haya tunaamini kwamba wabunifu watapata habari muhimu zitakazowawezesha kuchangia moja kwa moja ukuaji wa sekta ya ubunifu Tanzania”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaji wa Swahili Fashion Week.

Mafunzo hayo yataendeshwa na Claire Hamer-Stubbs ambae anatoka katika kampuni ya Ei8ht (www.ei8ht.org), kundi ambalo limekuwa likifanya kazi zake nchini Uingereza.

Warsha hiyo itafanyika katika Hotel ya New Africa kwa muda wa siku nne kuanzia Ijumaa ya tarehe 27 mpaka Jumatau tarehe 30 mwezi huu na kuwahusisha wabunifu 12 wa mavazi hapa nchini.

“TSDU kwa sasa tumeshirikiana na Swahili Fashion Week katika programu ya kuwasaidia wabunifu wa Tanzania kwa kutoa mafunzo ya awali , TSDU inaamini kwamba kwa kutoa fursa ya mafunzo kwa wabunifu ambayo yatawawezesha kutambua mpangilio mzima wa kufanya kazi zao.

Tunaamini kwamba kupitia semina hii wabunifu watajipatia uelewa mpana wa kufanya kazi na wanunuzi wa rejareja kutoka Uingereza ambao huenda wakavutiwa na bidhaa zinazozalishwa na wabunifu wa Tanzania. Alieleza Mark Bennet, mtaalamu kutoka viwanda vinavyotengeneza nguo vya hapa Tanzani.

Miongoni mwa maeneo yatakayofundishwa katika warsha hii ni pamoja na:

· Biashara na ubunifu, ambapo zaidi itagusia kufafanua ubunifu, mifano mbalimbali, gharama za uzalishaji.

· Masuala ya uzalishaji kwa ujumla, ambapo zaidi wataangalia vipengele vinavyohusu fedha, ufundi, ubora wa bidhaa na jinsi ya kufanya kazi na viwanda vingine vya uzalishaji.

· Ufundi katika ubunifu kwa mfano katika ufungaji, uwekaji wa lebo, maadili ya uzalishaji sambamba na mazingira ya kazi kwa ujimla.

· Watapata pia fursa ya kukutana na wanunuzi kutoka Uingeraza, na kujua ni bidhaa gani zinazohitajika Uingereza, pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na jinsi ya kufikia matarajio.

“Wabunifu wa Tanzania waitumie nafasi hii ipasavyo katika kujipatia mbinu tofauti za kutengeneza bidhaa zao, pamoja na kujipatia mbinu mpya za masoko kwa bidhaa wanazozalisha. Nafasi hii haitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja bali kwa sekta nzima ya ubunifu hapa nchini.” Alimazia Mustafa Hassanali.

No comments:

Post a Comment