header

nmb

nmb

Tuesday, August 31, 2010

MAAJABU YAZIDI KUENDELEA MASHULENI WANAFUNZI WAKUMBWA NA GONJWA LA AJABU!!


Wanafunzi waanguka mashetani

Na Khadija Idd, Tabata

VILIO na simanzi vimetawala leo katika Shule ya Msingi Tumani ambako zaidi ya wanafunzi 26 wameanguka ghafla na kuanza kupiga mayowe wakidai wanawaona watu walio uchi wa mnyama.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu tukio hilo limetokea leo saa 2 asubuhi ambapo wazazi na walezi walilazimika kutinga katika shule hiyo kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto wao.

Hali hiyo imezua tafrani kati ya wazazi na walimu hao ambapo kwa msaada wa haraka walikuwa wakiwachukua watoto wanaodondoka kisha kuwakimbiza kwenye kanisa la Assembles Of God lililopo jirani kwa ajili ya kuombewa.

Akizungumza na gazeti hili shuleni hapo, mwalimu wa shule hiyo, Frank Mtawa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limekuwa likijitokeza kila mwaka katika shule hiyo lakini mwaka huu limekuwa la aina yake.

Amesema leo asubuhi, wakati Mwalimu Godfrey Wilbard akifundisha darasani, ghafla alisikia mwanafunzi mmoja akipiga mayowe akidai kuwa anaona watu walioko uchi wa mnyama wakimwita, ndipo alipozirahi huku akifuatiwa na wenzake watano.

Amesema baada ya mayowe hayo wanafunzi wengine waliendelea kuanguka mfululizo na kusababisha walimu kutoa taarifa kwa wazazi na walezi ambao walifika mara moja kwa ajili ya kusaidiana kuwatuliza watoto hao.

Mwalimu Mtawa amesema hata hivyo hali ya mwanafunzi mmoja wa kiume na mbaya na wanaendelea na jitihada zaidi za kumsaidia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kuzungumzia zaidi tukio hilo.

No comments:

Post a Comment