header

nmb

nmb

Wednesday, August 4, 2010

KURA YA MAONI KENYA HADI MIDA HII HAKIJA ELEWEKA!!




Kenya wapiga kura kuamua Katiba mpya

NAIROBI,Kenya

WANACHI nchini Kenya leo wamepiga kura ya maoni itakayoamu rasimu ya katiba mpya,huku ukitolewa wito wa amani kote nchini humo.

Kura hizo za maoni zinafanyika ikiwa ni miaka miwili tangu mamia ya watu kuuawa katika ghasia zilizozuka punde baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007.

Katiba mpya imelenga kubadilisha mfumo wa siasa za Kenya na kuzuia kutokea tena kwa ghasia hizo zilizowaacha pia maelfu ya watu bila makao.

Kura ya maoni imeonyesha kuwa katiba hiyo itakubaliwa na wananchi.

Wanaoiunga mkono katiba wanasema kuwa itachangia ugawanaji wa mamlaka kwa kuunda utawala wa majimbo, kumaliza ukabila na pia kusuluhisha au kuleta mabadiliko katika sera ya ardhi.

miongoni mwa viongozi waliotoa wito wa amani wakati wa shughuli hiyo ni Rais Mwai Kibaki, Waziri Mkuu, Raila Odinga na viongozi wa Tume ya muda wa Uchaguzi nchini humo (IIEC).

No comments:

Post a Comment