Rais Somalia aongoza mashambulizi dhidi ya wanamgamboMAGADISHU,Somalia
WAKATI Somalia juzi iliazimisha kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru, imeelezwa kuwa Rais wa nchi hiyo,Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi wanamgambo wa Kiislamu.
Walioshuhudia waliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kuwa kiongozi huyo alikuwa amevaa mavazi ya kijeshi huku akiwa juu ya kifaru cha majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika AU.
Awali kabla ya maadhimisho hayo rais huyo alikuwa ametahadharishwa kuwa Somalia ipo hatarini kutoweka kama taifa.
Majeshi ya Serikali ambayo yanasaidiwa na walinzi wa amani kutoka Afrika wapo katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wanaoshikilia eneo kubwa la Somalia.
Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, Bw. Mohamed Moalimuu aliripoti kutoka katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu,akisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa rais kwenda mstari wa mbele kuongoza mashambulizi.
Ilielezwa kuwa mashambulizi hayo ya majeshi ya Serikali ni kutokana mapigano ya siku mbili kati ya kundi la kiislamu la al-Shabab na washirika wake ambao wanajaribu kurejesha eneo la Kaskazini mwa mji wa Mogadishu ambalo yamelipoteza siku za hivi karibuni.
Mwandishi huyo wa BBC aliripoti kuwa vikosi vya Serikali vilianza kuishambulia ngome ya wanamgambo hao iliyopo katika eneo la Karan ambayo ni makazi ya watu Jumatano jioni.
Kwa mujibu wa taarifa za maofisa wa hospitali, watu nane waliuawa na wengine 82 kujeruhiwa katika mapigano hayo ya jana.
Habari nyingine kutoka nchini humo zilieleza kuwa wakati mapigano hayo ya juzi yakiendelea kundi la wanamgambo la Hizbul-Islam ambalo ni mshirika wa kundi la al-Shabab katika mji wa Mogadishu liliamuru vituo vyote vya redio visitangaze vipindi vyovyote kuhusu mahadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.
Mwandishi huyo wa BBC aliripoti akisema kuwa vituo vingi vya redio vilikubali kutii amri hiyo isipokuwa vituo vya redio ya Serikali na kituo binafsi cha Redio Shabelle ambacho hivi karibuni kimerejeshwa katika maeneo yanayoshikiliwa na Serikali

No comments:
Post a Comment