header

nmb

nmb

Tuesday, July 6, 2010

SAKATA LA TANROADS SASA LACHUKUWA SURA MPYA!!


Akizungumza bungeni juzi, Waziri wa Miundombinu, Dkt. Shukuru Kawambwa, alisema suala hilo ni zito linalogusa hoja za kisheria, hivyo wizara yake itamhusisha pia Mwanasheria Mkuu kulipatia ufumbuzi.
Hatua hiyo ilikuja baada ya wabunge kuhoji malumbano yanayoendelea kwa muda mrefu sasa kuhusu mkataba wa mtendaji huyo na kutaka kupata msimamo wa serikali.
"Mheshimiwa Spika, kuhusu muda wa utendaji kazi wa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Serikali bado inalifanyia kazi suala hili na muda muafaka ukifikia basi tutalitolea maelekezo. Ni kweli kwamba kuna utata kati ya barua ambazo mikataba ambayo Mtendaji Mkuu yule anayo na hili ni suala la kisheria na ushauri wa kisheria lazima upatikane na Mwanasheria Mkuu wa Serikali lazima alitolee maelekezo suala kama hili.
"Kwa hivyo si suala lile ambalo Serikali inaweza kukurupuka tu na kufanya maamuzi ambayo hayana ushauri wa kisheria kutokana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Itakapofikia mwisho wa ufafanuzi wa jambo hili, Serikali haitakuwa na kigugumizi cha kuweza kulitolea kauli na kuchukua hatua zile muafaka" alisema Waziri Kawambwa.
Kuhusu mikataba ya baadhi ya mameneja wa TANROADS Dkt. Kawambwa alisema "Mheshimiwa Spika, kuhusu hoja ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS. Wizara ilikutana na Bodi ya TANROADS na Mtendaji Mkuu kama vile Kamati ilivyoagiza.
"Katika kikao hicho ilielekezwa ifuatavyo kwamba wafanyakazi waliokuwa na mikataba waendelee na kazi zao hii iliwahusu mameneja wa TANROADS wa mikoa 10 ambayo ni Ruvuma, Dodoma, Iringa, Morogoro, Arusha, Kagera, Shinyanga, Dar es Salaam, Mwanza na Tabora ambao wote walitakiwa kuachishwa kazi. Na Ofisi ya Bunge Dodoma

No comments:

Post a Comment