header

nmb

nmb

Thursday, July 15, 2010

MUSEVENI AAHIDI KUWATIA MIKONONI KUNDI LA AL-SHABAAB!!


RAIS Yoweri Museveni wa Uganda,ameapa kuwasaka na kuwamaliza wapiganaji wa al-shabaab waliofanya vitendio vya kiagaidi katika ukanda wa Afrika,

Museveni aliyasema hayo alipohutubia waandishi wa habari jana usiku katika mji wa Ntungamo mashariki mwa Uganda.

Aliongeza kuwa magaidi hao watasakwa nchini Uganda na pia nchini Somalia. Hii inafuatia taarifa iliyotolewa mapema wiki hii na kundi hilo la Al-Shabaab kuwa walihusika na shambulio la bomu mjini Kampala lililowaua zaidi ya watu 70.

Museveni pia alitoa wito wa kuongezwa majeshi ya kuweka amani ya muungano wa Afrika AU, kufikia 20,000 kukabili makundi ya wapiganaji nchini Somalia ambayo amedai yanapata ufadhili kutoka Mashariki ya Kati.

No comments:

Post a Comment