header

nmb

nmb

Thursday, July 15, 2010

MATUKIO YA KUVAMIWA BAA TARIME NA DAR KISHA KUUWAWA WATU WAWILI YATIA SIMANZI!!

PICHA NA HABARI ZAIDI CHINI

KUNDI la majambazi limevamia baa na kuwajeruhi wateja na kumuua mlinzi wa baa na kisha kuiba kreti za bia.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Matongo wilayani Tarime ambapo majambazi hayo waliwapiga wateja wa baa hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Costantino Massawe, amesema kundi la majambazi hao walivamia katika baa inayomilikiwa na Muhiri Mugaya na kupora Televisheni moja, fedha, na kreti za bia.

Amesema mlinzi aliyeuawa amefahamika kwa jina la Kenkya Wambura (54) na kuwajeruhi wateja waliokuwa wakinywa bia.

Amesema waliojeruhiwa kuwa ni Zakaria Nyamuya ambaye amepigwa risasi tumboni na kisha utumbo kutoka nje, mwingine ni Marwa Mugaya ambaye amevunjwa miguu yote na majambazi hao.

Kamanda amesema pia mhudumu wa baa hiyo, ambaye hakuweza kufahamika jina lake, amepigwa risasi mgongoni na pia mteja mwingine ambaye jina lake bado halijapatikana amepigwa risasi sehemu za makalio.

Amesema hali za majeruhi hao ni mbaya na wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Tarime na upelelezi unaendelea ili kuweza kuwanasa majambazi hao.

KATIKA TUKIO LA DAR
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sadam ameauwa kwa kupigwa risasi katika baa maarufu ya Angels' Park iliyoko Ilala Sharief Shamba jijini Dar es salaam!! Kijana huyo inadaiwa kuuawa na mmiliki wa bar hiyo baada ya kundi la vijana wengi, akiwemo marehemu, kuvamia kwa lengo la kumpiga mwenye baa ili kulipiza kisasi! Mtandao huu umeeleza na mashuhuda kuwa, sakata lilianzia jana baada ya vijana wasiojulikana kudaiwa kumkaba mteja mmoja wa baa hiyo akiwa chooni na vijana hao kukamatwa na kuplekwa polisi ambako walishikiliwa hadi leo. Imedaiwa kuwa baada ya kuona wenzao wanasota rumande, pengine kwa sababu ya mmiliki wa huyo, waliamua kumfuata ili kulipiza kisasi kwa kumfanyia. Wakiwa kundi huku wameshika silaha mbalimbali vikiwemo visu, vijana hao walivamia baa hiyo na kuanza kumpiga mwenye baa na kumchoma kisu ambacho bahati nzuri hakikumdhuru sana. Kuona hali hiyo, mwenye baa alitoa bastola yake, akapiga hewani ili kuwatisha, lakini waliendelea kumfuata na kumshambulia huku wakiharibu mali za baa hiyo, likiwemo gari lake lililovunjwa kioo cha nyuma. Awali vijana wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa na marehemu aliendelea kumfuata mwenye baa na ndipo alipopigwa risasi na kufa papo hapo! Habari globapublisher
Gari ya Mmiliki wa baa iliyovamiwa na kuvunjwa vioo.

Baadhi ya watu waliojitokeza kushangaa tukio hilo jana

No comments:

Post a Comment