header

nmb

nmb

Tuesday, July 20, 2010

KANARI GADAFI AOMBA AMANI IPATIKANE MEZANI!!




KIONGOZI wa Libya,Muammar Gaddafi ametoa wito kwa kiongozi wa waasi nchini Sudan, Khalil Ibrahim ambaye kwa sasa anahifadhiwa na Serikali ya Tripoli kurejea katika mazungumzo ili kutafuta amani.
"Natoa wito kwa kaka yangu Khalil kurejea katika majadiliano ya mjini Doha kwa sababu hakuna maamuzi mengine bali ni kurejea katika mchakato huo wa kutafuta amani.
Kanali Gaddafi alikiambia kituo cha Radio France International.

Ibrahim ni kiongozi wa kundi la Justice and Equality Movement (JEM), ambalo ni kubwa katika Jimbo la Darfur.

Kwa sasa kiongozi huyo yupo nchini Libya tangu Mei 19, baada ya kurejeshwa nyumbani na Serikali ya Chad wakati akijaribu kuingia jimboni Darfur.

Kundi la JEM lilijitoa katika mazungumzo ya amani mwezi Mei ambayo yanaihusisha Serikali ya Qatar,Umoja wa Afrika AU na Umoja wa Mataifa UN.

Uamuzi wa Libya kumpatia hifadhi Ibrahim ulijiwa juu na Serikali ya Khartoum ambayo inatafuta muafaka na kuwaomba Polisi wa kimataifa Interpol kusaidia kukamatwa kwake.

Katika mahojiano na kituo hicho cha redio, Kanali Gaddafi alisema kuwepo kwa sasa Ibrahim kunaiweka njia panda Tripoli na akaongeza kuwa kwa sasa wamempiga marufuku kutoa amri ama kutoa taarifa yoyote akiwa nchini humo.

"Sitetei upande mmoja dhidi ya mwingine,jukumu langu siyo kutetea bali ni kutafuta suluhu kati ya pande zote mbili husika ,"alisema Kanali Gaddafi.

Kanali Gaddafi alisema kuwa pia kuna mazungumzo mazungumzo kati ya Ibarahim na Rais wa Chad, Idriss Deby Itno yanayofanyika nchini Libya lakini hakutoa taarifa zaidi.

Umoja wa Mataifa UN unakadiria kuwa watu takribani 300,000 wameuawa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe jimboni Darfur iliyodumu kwa takribani miaka saba na wengine milioni 2.7 wamekimbia makazi yao. By. BBC

No comments:

Post a Comment