header

nmb

nmb

Tuesday, July 20, 2010

INAELEKEA MAKONGORO MAHANGA HATAKIWI TENA TABATA NI BAADA YA KUTOLETAMAENDELEO UKONGA NA KUHAMIA JIMBO LA SEGEREA!!






MBUNGE Mstaafu Makongoro Mahanga akisaini fomu ya kuomba kugombea tena jimbo la Segerea

KWA kile kinachoashiria huenda kampeni za mwaka huu zikawa za kukata na shoka Wana-CCM zaidi ya kumi wamejitokeza kumkaba koo Mbunge anayetetea nafasi yake,Makongoro Mahanga ambaye ni Naibu Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana ambaye anawania jimbo hilo jipya baada ya kuliacha lile la Ukonga hali inayoonyesha hatakiwi tena.

Wakiongea na blog hii baadhi ya wagombea wamedai kuwa watamgalagaza kwa kutumia Kigezo cha Madai ya DIGRII FEKI ILIYODAIWA NA MWANAHARAKATI MSEMAKWELI

Kwa mujibu wa waandishi wa blog hili waliotembelea katika vituo mbalimbali vya kuchukulia fomu hizo leo asubuhi, wamesema kuwa, hadi sasa ni wagombea 21 wamejitokeza kuwania nafasi za Ubunge kwa jimbo la Ukonga, Segerea na Ilala.

Wakati hao tayari wakielekeza silaha zao ndani ya siasa tayari kwa kujifua na wakongwe wengine wa siasa baadhi ya wagombea wengine zaidi ya watano wameonesha nia ya kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania jimbo la Segerea.

Waliochukua fomu katika Jimbo la Segerea hadi sasa ni nane, Ilala watatu, Ukonga 11 huku wengine 35 wakijitokeza kuwania nafasi ya Udiwani viti maalum ambapo wanane wamerejesha fomu hizo.

Jimbo la Temeke hadi leo asubuhi ni wagombe wanane wamejitokeza kuwania nafasi ya Ubunge akiwemo Mbunge anayetetea nafasi hiyo, Tambwe Hizza, Mbunge wa zamani, Khadija Kusaga, Salim Chicago na Moud Nando.
Wakati kwa Jimbo la Kawe waliochukua fomu za Ubunge ni 16 ambapo baadhi yao ni Faustine Kikove, Mahamoud Madenge, Nicodemus Chengula, Erick Suma, Omary Wahure na wengineo.

Hadi leo asubuhi Wilaya ya Ilala ni wagombea wanne wa Ubunge ambao tayari wamerejesha fomu hizo kwa ajili kuomba ridhaa katika mchakato huo ambao ni Mbunge wa zamani, Mussa Zungu anayetetea nafasi yake, Japhary Ole Koimale, Magaya Gasaya na Eugen Mwaiposya.

Kwa wakazi wa jiji la DSM Habari hii waweza kuipata zaidi katika Gazeti la Dar leo

No comments:

Post a Comment