header

nmb

nmb

Tuesday, July 20, 2010

DEZO YA POMBE YAMPONZA MSKAJI BUNGURUNI DAR ES SALAAM!!

PICHA HII NI MFANO WA TU JAMAA HUYO HAKUWEPO KIKAO HICHI

MKAZI wa Vingunguti Ally Idd (19),amefikishwa katika Mahakama
ya Mwanzo Buguruni kujibu mashitaka ya kujipatia huduma za
vinywaji vya bia na sigara dezo.
Mshitakiwa amesomewa mashitaka yake na karani Hyasinta Mambo
mbele ya Hakimu Adelf Sanchore wa mahakama hiyo.
Imedaiwa kuwa Mei 17, mwaka huu, saa 4 asubuhi , Vingunguti
Mtambani, mshitakiwa alifika katika baa ya mlalamikaji Mwikwabi
Werema.
Na kuagiza bia tano aina pamoja na sigara kumi vyote vikiwa na
thamani ya sh. 8,000 huku akijua hana mapene ya kupei
Hata hivyo mshiakiwa amekana mashitaka na kesi yake itatajwa
tena Julai 30, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment