header

nmb

nmb

Friday, July 16, 2010

BUNGE LA TANZANIA LINAKWISHA LEO!!


WAKATI Rais Jakaya Kikwete na jopo la viongozi wenzake la wakuu wa nchi akitarajia kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mchakato wa kulivunja baada ya kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka mitano, hekaheka za wabunge zimeanza katika majimbo mbalimbali huku wengine wakiwa na mashaka ya kutorudi tena katika wadhifa huo.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya wabunge wameanza kuhaha kuomba ridhaa ya wananchi ya kuwarudisha tena bungeni, hali ambayo inawapa ugumu baadhi ya wabunge ambao wanaonyesha dhahiri kuwa tangu walipoonana na wapiga kura wao wakati wakiomba kura ndiyo wanarejea tena kuombwa kura.

Hali hiyo imewapa hofu baadhi ya wabunge na madiwani ambao wengi wao wameyakimbia majimbo na kata zao huku wengine wakizihama kuhofia kubwagwa kwa kishindo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kutekeleza ilani za uchaguzi wa vyama vyao wakati wa kampeni zao.

Baadhi ya wabunge ambao wanahofia kubwagwa ni wale wa majimbo ambayo baadhi ya wananchi wenye sifa wameibuka na kutangaza nia ya kugombea nafasi hizo.

Rais Kikwete amewapongeza wabunge kwa kutoa michango mbalimbali ndani ya bungeni na kuwataka wawe wabunifu katika utendaji ili kuibadili nchi kiuchumi na kuwa na maendeleo.

Wakati huo huo, Chrisant Mzindakaya, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kwela mkoani Rukwa, ni miongoni mwa wabunge waliotangaza kung'atu kwa kile alichodai kuwa ni uamuzi wake wa dhati ambapo ameamua kufanya hivyo baada ya kulitumikia bunge zaidi ya miaka 40, ukuu wa mkoa kwa miaka 10 na Unaibu Waziri kwa miaka minane.

Mbunge huyo ametangaza nia hiyo na kuvitupia dongo zito vyama vyote vya siasa kuwa vinanuka rushwa.

No comments:

Post a Comment