Mbunge wa Afrika Mashariki Dkt. Didas Masaburi akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanachama wa shina la Wanamazingira Kata ya Kivukoni jana baada ya kufungua tawi kwa kukata utepe na kupandisha bendera.
Pia Dkt. Masaburi alizindua Umoja wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) na kuwaasa vijana hao cha Umoja huo kisiwe cha kukaribisha wezi,wavuta bangi na wauza madawa ya kulevya. Aliwakumbusha kuwa Kata hiyo ndiyo kitovu cha nchi kwa sababu ndiko Rais (Ikulu) iko katika kata hiyo ya Kivukoni.
HABARI YENYEWE.
MBUNGE wa Afrika Mashariki Dkt. Didas Masaburi amewataka vijana wa CCM kuacha kugeuza mashina ya wakareketwa kuwa vijiwe vya wavuta bangi na vyanzo vya uhalifu.
Akizungumza juzi wakati akizindua tawi la Wanaharakati wa Mazingira Kivukoni, Dkt.Masaburi alisema vijana ni tegemeo la taifa katika kuzalisha uchumi na kuonesha mwelekeo wa taifa hivyo sifa mbaya ya wizi, ujambazi na ulevi isipewe nafasi kwa vijana wa CCM.
Alisema baadhi ya watu wanapaka matope mashina ya wakereketwa kuwa wanajihusisha na uhalifu hivyo wachache wasiokuwa na maadili mema wanatumia nafasi hiyo kuwavurugia wenzao na kupaka matope CCM.
Dkt. Masaburi ambaye ni Kamanda wa Vijana wa CCM Wilaya ya Ilala alisema imefika wakati kwa vijana kuungana katika vikundi kuanzisha miradi ya kiuchumi ili kuvutia wawekezaji ambao watakubali kuwekeza kama watakuta mazingira yanavutia.
Alisema tawi la Wanaharakati wa Mazingira wa Kivukoni wanao wajibu wa kupendezesha eneo hilo liwe safi na livutie watalii ambao wanapenda kutembelea eneo hilo kabla ya kwenda mikoa mingine nchini kutalii.
Dkt. Masaburi alilitaka shina hilo lipambane na magonjwa ya kuambukiza ya kipundupindu yanayotokana na uchafu kwa kufanya usafi wa mifereji na kusomba takataka katika eneo hilo ambalo ndiko ilipo ofisi za viongozi wa juu wa nchi.
Aliwashauri vijana wote kujiandaa kupigia kura CCM katika uchaguzi Mkuu ujao ili madiwani, wabunge na Rais wachaguliwe kutoka chama hicho kwa kura ya zaidi ya asilimia 99.Imetayarishwa na Peter Mwenda wa majira News Paper

No comments:
Post a Comment