MFANYABIASHARA Ally Ramadhani (29), mkazi wa Kigogo, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.
Mbele ya Hakimu Suzan Kihawa imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Benedict Nyagabona kuwa Mei 9, mwaka huu, mshitakiwa alimbaka mwanafunzi huyo.
Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Juni 19, mwaka huu.
Pia, Suma Nangoma (20), mkazi wa Mwananyamala, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu mashitaka ya kukutwa na bangi.
Imedaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alikutwa na askari E.1090 Koplo Thausen alipokuwa doria maeneo hayo.
Mbele ya Hakimu Mary Matoi imedaiwa na Karani Fatma Khatibu kuwa, mshitakiwa alikamtwa akiwa na bangi.
Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Juni 19, mwak
No comments:
Post a Comment