header

nmb

nmb

Wednesday, June 16, 2010

MASIKINI DOGO HUYU DAKATARI FEKI WAOZESHA ENEO NYETI LA!!



MTOTO mwenye umri wa miaka minne anauguza kidonda kikubwa sehemu ya makalio baada ya kudungwa sindano na madaktari ambao wanasadikika kutokuwa na utalaamu wakijaribu kumtibia homa.
Habari kutoka Kampala zimeeleza kuwa kwa muda wa miezi minne mtoto huyo, Immaculate Nanyonjo amekuwa akilala kitandani kutokana na kuwa hawezi kukaa baada ya sehemu kubwa ya kalio lake la kushoto kuoza na kubakia na shimo kubwa.

“Jeraha hilo limesababisha shimo na linatishia mfupa kutokana na kuwa kubwa na refu, nadhani itakuwa saratani,” alisema diwani wa Wilaya Buyende, Aisha Kanaku wakati alipoitembelea familia hiyo Jumapili iliyopita.
Imeelezwa kuwa Nanyonjo ambaye ni mtoto wa familia ya Stephen Muzaale na Elizabeth Nabutono wakazi wa kijiji cha Kiribairya alianza kupata matatizo hayo baada ya kupelekwa Zahanati mbalimbali za watu binafsi na kuchomwa sindano ili kumtibia homa.
Hata hivyo baada ya kudungwa sindano hizo mtoto huyo aliendelea kupata homa huku upande alipochomwa sindano ukivimba.
Nanyonjo na ndugu zake wengine nane kwa sasa wanaishi chini ya uangalizi wa bibi yao mwenye umri wa miaka 80 baada ya mwaka 2008 mama yao kutengana na baba yao na kisha mwanamume huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye anaishi naye nyumba tofauti.
Bibi wa watoto hao, Kotirida Ikesa alimwambia diwani huyo kuwa mtoto huyo alichomwa sindano katika Zahanati zilizopo jirani na nyumbani kwao lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya hivyo kulazimika kumpeleka kwa madaktari wengine wawili wanaondesha maduka ya kuuza madawa ambao walimchoma sindano kadhaa ambazo zilimsababishia kuvimba zaidi.
Alisema, baada ya hali hiyo kuzidi walimpeleka mtoto huyo wa kike katika hospitali ya Kamuli ambapo alifanyiwa upasuaji na daktari ili kuondoa uvimbe na baada ya upasuaji huo Nanyonjo alihamishiwa hospitali ya Mulago iliyopo jijini Kampala kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

“Tulilipa sh. 200,000 kwa ajili ya matibabu katika hospitali Kamuli tukaishiwa fedha hivyo tukashindwa kwenda Mulago na badala yake tukaanza kutumia dawa za asili ambazo ni mifupa ya samaki ya kuchoma iliyochanganywa na magamba ya mti wa Mvule,”alisema Nabutono mama ambaye anamuuguza mtoto huyo.
Nabutono alisema kuwa mumewe ambaye amemtelekeza amekwishatangaza kuwa hawezi kutumia fedha zake kwa ajili ya kutibia ugonjwa usiopona.
“Sina kipato na hatimaye mwanangu atakufa,”alieleza Nabutono ambaye amerejea katika nyumba yake ya zamani ili kumuuguza mwanaye.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Buyende,Dkt. Aggrey Batesaaki, madaktari waliomtibia mtoto huyo awali huwenda walitumia dawa zilizokwisha muda ama hawana utaalamu na akasema kuwa mtoto huyo atapona endapo atapata uangalizi wa wataalamu.

Kwa mujibu wa wanaharakati wa kutetea Haki za Budamu, utoaji huduma kwenye zahanati binafsi zisizo kuwa na wataalamu kumekuwa kukichangia ongezeko la idadi ya watoto wenye ulemavu nchini Uganda.
Wanaharakati hao wanasema kuwa kesi nyingi za watoto kuwa walemavu ni baada ya kudungwa sindano na dawa zisizofaa.

bbc Unganda

No comments:

Post a Comment