header

nmb

nmb

Friday, June 4, 2010

AUWAWA AKIWA NA JAMBO ZITO MOYONI!!


Mwanaharakati wa Haki za Binadamu auawa DRC
KINSHASA,Kongo DRCMWANAHARAKATI wa Kutetea haki za Binadamu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC, Floribert Chebeya amepatikana ameuawa viungani mwa mji mkuu wa Kinshasa.
Maiti ya Chebeya ilipatikana ikiwa imefunikwa kwa nguo kwenye kiti cha nyuma cha gari lake.
Imeelezwa kuwa Chebeya amewahi kukamatwa na kuteswa na polisi, na kabla ya kuuawa kwake alitarajiwa kufika mbele ya mkuu wa polisi wa Kinshasa juzi.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limeelezea kushtushwa na mauaji hayo ya Chebeya ambaye ni mwanaharakati aliyesifika na kuheshimiwa sana nchini DRC.
Kwa mujibu wa shirika hilo, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini humo wamekuwa wakiteswa sana baadhi wakitishwa na hata kukamatwa kiholela.

No comments:

Post a Comment