header

nmb

nmb

Thursday, May 6, 2010

wanamgambo wavamia hospitali kwa risasi...!!WANAMGAMBO wa Kiislamu wa kikundi cha Hisbul-ul-Islam nchini Somalia katika mji wa mkuu Mogadishu, wameshambulia hospitali ya Afgoye iliyopo nje kidogo ya mji huo.

Imeelezwa kuwa sababu ya hsambulio hilo ni kulipiza kisasi kutokana na mauaji ya kamanda mmoja wa kundi hilo ambaye aliuawa hivi karibuni kutokana na mapambano makali yaliyofanyika katika mji huo.

Waliamua kufikia hatua hiyo kutokana kwa madai ya kuwashutumu walinzi wa hospitali hiyo kuwa ndio waliotenda mauaji hayo ya kiongozi wao hivyo ilikuwa ni halali kwa kulipiza kisasi.

Pamoja na kuwapo kwa madai hayo, madaktari wa hospitali hiyo wamesema hawakuwa na taarifa zozote kuhusu kiongozi wa kundi hilo na kama alishawahi kufika katika hospitali hiyo.

Katika mashambulizi yaliyotekelezwa na wanamgambo hao, mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa na kwamba mashambulizi hayo yamerudisha nyuma juhudi na usalama wa wafanyakazi na raia katika hospitali na maenekatika hayo.

Hospitali hiyo pia inajishughulisha na kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

Somalia inatajwa kuwa ni moja ya nchi mbaya na hatari katika utekelezwaji wa kazi ya uandishi wa habari.

Jumanne wiki hii watu wenye silaha walimvamia na kumuua mwanahabari maarufu nchini humo aliyekuwa akifanya kazi katika radio ya Taifa mjini Mogadishu.

Mwanahabari huyo, Shehe Nur Abkey, alitekwa nyara Jumanne na watu wasiojulikana na kumpeleka kusikojulikana ambapo jioni ya siku hiyo mwili wake ulitupwa na wauaji kutokomea.

Mpaka sasa bado haijajulikana wazi nani aliyemuua lakini wanahabari wenzake wanasema aliuawa kwa sababu alikuwa mfanyakazi wa Radio Mogadishu ambayo hukosoa vikali mienendo ya wanamgambo wa Kiislamu.

Hata hivyo, bado upelezi uanendelea na kwamba hakuna matumaini yoyote ya kukamatwa kwa wauaji hao kutokana na ugumu uliopo nchini humo katika kuwafuatilia watu walihusika katika mauaji ya mtu yoyote.

No comments:

Post a Comment