header

nmb

nmb

Wednesday, May 12, 2010

WANAFUNZI SUA MOROGORO WAUWA MLINZI WAO KWAKUMFICHA MWIZI WA SIM!!

Jengo la Chuo kikuu cha SUA

VURUGU ziilibuka katika Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na kusababisha mlinzi wa chuo hicho, Jafari Thabit (38), kupigwa na wanafunzi na kuuawa baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali.
Vurugu hizo zilianza baada ya mwanafunzi wa kike anayeishi katika hosteli ya chuo hicho kupotelewa na simu yake ya mkononi.
Wakati mlinzi huyo anayetoka katika kampuni ya ulinzi ya Moku na mkazi wa Chamwino akiendelea na kazi yake ya ulinzi, ghafla kundi la wanafunzi lilimvamia kwa tuhuma kuwa ndiye aliyeiba simu hiyo.
Kundi la wanafunzi hao limedaiwa kuwa lilimshambulia mlinzi huyo kwa kumpiga na kumjeruhi kichwani na kitu chenye ncha kali.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Thobias Andegenye, amesema tukio hilo lililotokea katika hosteli za Mazimbu ambapo wanafunzi hao walimpiga na kumjeruhi mlinzi huyo. Kamanda Andengenye amesema mlinzi huyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa lakini alifariki wakati akiendelea kupata matibabu.
“Tulifika eneo la tukio na kumkuta mlinzi huyo akiwa amejruhiwa vibaya, hivyo alichukuliwa na kukimbizwa hospitalini. Hata hivyo alifariki akiwa anaendelea kupata matibabu,” amesema kamanda.
Amesema kutokana na tukio hilo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda amesema wanafunzi waliohusika na kitendo hicho walitoweka mara baada ya tukio lakini juhudi zaidi zinaendelea za kuwasaka wanafunzi hao.
Amesema wanafunzi sita wanadaiwa kuhusika na tukio la mauaji hayo na jeshi lake linaendelea kuwasaka na mara watakapokamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.By.NIKSOON MKILANYA

No comments:

Post a Comment