header

nmb

nmb

Friday, May 7, 2010

MWITO WATOLEWA KUHUSU MAJI KATIKA MAZIWA YETU NCHINI!!

Uchafuzi nauharibifu wa mazingira katika Ziwa Nyasa umepelekea kina cha maji katika bandari ya Itungi kupungua na hivyo meli kushindwa kufika kupaki kama inavyoonekana pichani,Gari aina ya fusso likionekana likishusha mizigo na kupakia katika mojawapo ya boti ambayo yanapelekwa eneo ambalo meli zimekuwa zikitia nanga upande wa bandari ya kiwira.
WATANZANIA wametakiwa kuomba vibali vya utumiaji maji hadi kufikia mwaka 2011 baada ya hapo watakuwa wamekiuka sheria ya rasilimali za maji na kuhesabika kuwa wanavunja sheria na hivyo kufikishwa katika vyombo husika.
Mwito huo umetolewa na Kaimu Ofisa maji Bonde la Ziwa Nyasa,Witgal Nkondola wakati akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilkaya ya Mbozi,Levisson Chillewa,katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya wawezeshaji (DFTs) ya wiki tatu iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi,jana.
Nkondola alisema watumiaji wa maji ama watarajiwa, wanapaswa kuomba mapema vibali vya kutumia maji kwa mujibu wa sheria ya rasilimali za maji na.11 ya mwaka 2009 kifungu na.43(1) ambapo sheria imetoa fursa ya wote ambao kwa sasa hawana vibali hivyo na wanatumia maji kuomba kupatiwa. "Ili kuleta ufanisi katika suala zima la matumizi ya maji,napenda kuchukua fursa hii kuziomba halmashauri na Ofisi za bonde kufanya kazi kwa ukaribu zaidi kwa kuimarisha mawasiliano,kushirikiana bega kwa bega na kwa niaba ya Ofisi natoa mwito kwa watumiaji wa maji na wale watarajiwa kuomba vibali mapema ndani ya miaka miwili baada ya hapo watakuwa wanavunja sheria,"alisema.
Ofisa huyo amezitaka halmashauri,wilaya na miko kwa kushirikiana na Ofisi za mabonde kusimamia utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji,matumizi bora na endelevu ya rasilimali maji kwa kuwashirikiasha wadau mbalimbali wa matumizi ya maji.
Aidha Nkondola alisema jumla ya washiriki 36 kutoka katika Wilaya ya Mbozi,Njombe,Ludewa,Makete,Songea,Mbinga,Kyela,Ileje,Namtumbo na Rungwe wamepatiwa mafunzo ya uwezeshaji ambapo walianza kupatiwa mafunzo ya njia ya nadharia wilayani Kyela tangu aprili,11 hadi 23 ambapo mafunzo kwa njia ya vitendo walipatiwa kuanzia aprili,24 hadi 30 katika vijiji ambavyo kuna vyanzo vikuu vya mto Songwe unaopeleka maji Ziwa Nyasa navyo ni Idiwili,Ilomba,Hezya na Haraka Wilayani ya Mbozi.
Hata hivyo amebainisha mafunzo waliyopatiwa wataalamu hao ni pamoja na sera ya maji ya taifa,sheria mpya ya maji ya mwaka 2009,Uongozi shirikishi wa rasilimali za maji,ushirikishwaji wa wadau,mipango shirikishi ya maji,mafunzo shirikishi kwa vitendo,mbinu na vifaa,uchambuzi wa wadau,uchambuzi na utambuzi wa mti wa matatizo,mambo ya jinsia katika matumizi ya maji pamoja na mbinu za kuanzisha vyombo vya jumuiya za watumiaji maji.
By Thamasi Mpanji wa Jiji la Mbeya aliyetembelea huko

No comments:

Post a Comment