header

nmb

nmb

Tuesday, April 20, 2010

VIHIYO WA VYETI SASA KUKOMESHWA, KILA CHETI CHA MUHITIKU KITAWEKWA PICHAYAKE!!


DodomaSerikali kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania imeanza kuweka picha katika vyeti vya matokeo ya kidato cha nne na sita ili kudhibiti kutumiwa na watu wasio watainiwa kwa ajili ya kutafuta ajira au nafasi za masomo ya juu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza alisema hatua hiyo ya kuweka picha katika vyeti itawawezesha wadau kumtambua mmiliki halali wa cheti.
Aidha Mheshimiwa Maiza alisema zoezi la kuweka vyeti hivyo picha huwekwa kwa komputa hivyo picha hizo haziwezi kuondolewa.
Pia alisema zoezi la kuweka picha katika vyeti litaanza na vyeti vya watahini waliofanya Mtihani wa kidato cha nne mwaka 2008 ambavyo vitachapwa mwezi Mei 2010Naibu Waziri alisema hati ya matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2009 zimetolewa zikiwa na pichaAkijibu swali la nyongeza Waziri Maiza alisema serikali haian taarifa ya kubadilishana vyeti kwa wahusika kwani jambo hilo huwa hufanyika kwa makubaliano maalumu kati ya mwenye cheti na nayetaka kupew cheti hicho.
Hat hivyo Naibu Waziri Mahiza aliongezea kuwa Serikali imewakamata na inaendelea kuwakamata wale wote waliofoji vyeti na kuwafikisha katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi za kisheria .
Alitoa wito rai kwa wananchi wote kuacha mtindo wa kutumia vyeti visivyokuwa vyao kwani
kwa kufanya hivyo kunawanyima haki wenye vyeti stahili zao na ni kutenda kosa la jinai.
Imetumwa na Ofisi ya Maelezo Dodoma

No comments:

Post a Comment