header

nmb

nmb

Saturday, April 17, 2010

SIKIA HII NINOMA JAMAA YANGU!

Katekista jela kwa kumnajisi mpwa wakeKAMPALA,Uganda
KATEKISTA wa parokia ya Kasswa wilayani Kabarole nchini Uganda amehukumiwa kifungo cha muda mrefu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mpwa wake mwenye umri wa miaka mitano.

Bw.Joseph Mugasa ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka 17 jana aliongezewa adhabu hiyo na kuwa kifungo cha miaka 25 baada ya Mahakama ya Rufaa kutengua maamuzi ya Jaji Lameck Mukasa wa Mahakama Kuu ya Kabarole aliyoyatoa Februari 25, 2003.
Wakitoa hukumu hiyo Majaji, Amos Twinomujuni, Steven Kavuma na Augustine Nshimye walisema kuwa Jaji Mukasa alimuonea huruma Bw. Mugasa kwa kosa hilo ambalo alistahili kuhukumiwa adhabu ya kifo.

Kabla ya hukumu hiyo Mwanasheria Mkuu Serikali, Bw. David Ndamurani,alitaka mtuhumiwa achukuliwe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wanaotaka kufanya makosa kama hayo.

“Ni Katekista na vilevile ni mlinzi wa tabia katika jamii ambaye alitakiwa kuwa mfano mzuri na mlinzi wa watoto lakini badala yake anafanya kitendo kama hiki,” alisema Bw. Ndamurani.

Hata hivyo Jaji Twinomujuni alimshauri Bw.Mugasa kukata rufaa Mahakama Kuu endapo kama hakubaliani na maamuzi hayo.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi watoto wa kike wapatao 7,360 wamenajisiwa nchi nzima katika kipindi cha mwaka jana.

No comments:

Post a Comment