Katika Hali isiyo ya Kawaida Mshambuliaji wa Man U , W . Rooney ameomba mashabiki duniani kote kumuombea apone mguu wake haraka .
Mshambuliaji huyo muhimu aliumia mwishoni mwa mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Manchester United ilipopambana na Bayern Munich na kufungwa mabao 2-1 .
Rooney aliumia katika Uwanja wa Allianz Arena na alitoka uwanjani huku akichechemea baada ya kuumia enka, leo anatarajiwa kufanyiwa kipimo cha 'MRI scan' ili kuona ameumia kwa kiasi gani.
Habari hizo ni za masikitiko kwa kocha wa England, Fabio Capello ambaye anamtegemea mchezaji huyo katika kombe la Dunia na pigo kwa United ambayo inamtegemea katika mashindano hayo na ya Ligi Kuu England.
Mashetani Wekundu hao wanaweza kumkosa Rooney katika mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu dhidi ya mahasimu wao wa mbio za kuwania ubingwa Chelsea.
Inaonekana kuna nafasi ndogo kwa Rooney kuwa fiti kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Bayern Jumatano ijayo baada ya United kufungwa bao 2-1 ,huku Ivica Olic akifunga goli la ushindi dakika 93.
Rooney alianguka uwanjani na kugugumia maumivu baada ya kugongana na mshambuliaji wa Bayern aliyeingia kipindi cha pili, Mario Gomez.
wakati wa kutoka uwanjani alisaidiwa kwa kushikiliwa na wachezaji wenzie, kama atakuwa ameumia katika kiungio cha enka anaweza kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita, ambapo atakosa mechi zote hadi mwisho wa msimu.
Kocha wa United Alex Ferguson alisema: "Wayne Ameumia katika enka yake,ni mapema kuzungumzia kuhusu hali yake lakini tutajua kesho(leo).
Capello na nchi nzima itakuwa ikisali kuomba maumivuvu hayo yasimkose Rooney michuano ya Kombe la Dunia, ambapo imebakia miezi miwili tu kuanza.
Hiyo ni mara ya 12 kwa Rooney kuumia enka katika uchezaji wake, pia mchezaji huyo amekuwa akikabilwia na maumivu ya goti.
Rooney ndiye alianza kuifungia United bao la kwanza dakika ya pili, lakini pia alichangia goli la kusawazisha la Bayern baada ya mpira uliopigwa na Franck Ribery kumbabatiza na kumpotezea maboya kipa Van de sar kabla ya Olic kufunga goli jingine dakika za majeruhi.
BBC
No comments:
Post a Comment