header

nmb

nmb

Tuesday, April 13, 2010

MUZIKI MARUFUKU REDIONI NCHINI SOMALIA!!


Vituo vingi vya Redio nchini Somalia vimeacha kupiga muziki kwa amri ya wanaharakati wa kundi la Islamist Hizbul-Islam waliosema nyimbo ni kinyume na Uislamu.
Vituo hivyo vya Redio vimesema imewabidi watekeleze maagizo hayo kwa usalama wao.
Mwandishi wa BBC nchini Somalia amesema amri hii mpya ina baraka kubwa kutoka kundi la Taliban nchini Afghanistan.
Siku za nyuma, wanaharakati hao wa Kiislamu katika baadhi ya maeneo walipiga marufuku watu kuangalia filamu na mchezo wa mpira wa miguu na kuwalazimisha wanaume kufuga ndevu.Tangu mwaka 1991 Somalia imekuwa haina serikali imara na tangu wakati huo wanaharakati wa Kiislamu wamekuwa wakidhibiti maeneo mengi ya nchi.
Serikali ya mpito ya Somalia inayoungwa mkono na majeshi ya Muungano wa Afrika chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa wanadhibiti sehemu ndogo tu ya mji mkuu Mogadishu. http://www.bbcswahili.com/

No comments:

Post a Comment