header

nmb

nmb

Friday, April 16, 2010

MKUTANO WA PILI WA MAWAZIRI KUHUSU UDHIBITI WA MAAFA KATIKA BARA LA AFRIKA, 14-16 APRILI 2010, UMEKWEISHA LEO NAIROBI, KENYA

Mhe. Dkt. Batilda (mstari wa mbele, mwenye mtandio wa njano) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano huo uliohudhuriwa na nchi zipatazo 40 kutoka barani Afrika.
Mhe. Dkt. Batilda S. Burian (MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) akichangia mada katika Mkutano wa Pili wa Mawaziri kuhusu Udhibiti wa Maafa katika Bara la Afrika, uliofanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 14-16 Aprili 2010. Katika mada yake, alibaini ambavyo mabadiliko ya tabianchi yanachangia katika kuleta majanga ikiwemo mafuriko, kuenea kwa hali ya jangwa na magonjwa. Hivyo, alisisitiza umuhimu wa kujumuisha masuala ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na udhibiti wa maafa kwa mtazamo mpana zaidi na kwa kuzingatia masuala mtambuka yakiwemo ya jinsia, umaskini, hifadhi ya mazingira na utamaduni na mila. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuweka na kutekeleza mikakati madhubuti kwa kuwa vizazi vijavyo havitatuhukumu kwa yale tuliyofanikiwa bali kwa yale tuliyoshindwa kutekeleza.


No comments:

Post a Comment