header

nmb

nmb

Tuesday, April 27, 2010

CHUO SASA KIKO WAZI NENDENI MKASOMEE KUPAMBA MAHARUSI!!

MKURUGENZI WA MAZNATI SALOON

Chuo cha Maznat Vocation Training centre kilichopo Mikocheni B karibu na kanisa la mama Rwakatare nyuma ya redio Clouds kimefunguliwa hivi karibuni kwa ajili ya kuwakomboa wanamitindo wa Tanzania pamoja na wajasiriamali wa saloon.Mkurugenzi wa Maznat Vocation centre Maza Sinare amesema chuo kinatoa mafunzo ya kutengeneza kucha, nywele, ngozi na kupamba maharusi pia wanatoa mafunzo ya kiingereza bure ili kuweza kukabiliana na soko la Afrika mashariki linalokuja kwa kasi.Chuo hicho kitatoa mafunzo kwa ngazi ya Cheti( Certificate ) na bei zake ni poa na za kizalendo. Maza Sinare ameamua kuanzisha chuo hicho ili kuwakomboa wajasiriamali ambao wengi wao ni wanamitindo baada ya kutembea na kujifunza mengi ktk nchi nyingi za Ulaya na Afrika ya Kusini.
Kwa mawasiliano zaidi:
0713 88 18 52
prhabari@gmail.com

No comments:

Post a Comment