header

nmb

nmb

Saturday, April 10, 2010

BREKINGNIUZZZZZAJARI MBAYA YA NDEGE YAMUUWA RAIS!!


Rais wa Poland afa kwenye ajali ya ndege
MOSCOW,Urusi


RAIS wa Poland Bw. Lech Kaczynski na watu wengine kadhaa wanasadikika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka nchini Urusi wakati akijaribu kutua.


Maofisa katika Jimbo la Smolensk walisema kuwa hakuna abiria hata mmoja aliyesalimika katika ajali hiyo ya jana baada ya ndege kugonga mti.


Walisema kuwa maofisa waandamizi wa Serikali akiwemo mkuu wa jeshi wanasadikka kuwa miongoni mwa abiria waliokuwa katika ndege hiyo.


Kiongozi huyo alikuwa nchini Urusi kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya mauaji ya Katyn wakati majeshi ya Soviet yalipowaua maelfu ya Wapoland.
Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC,Bw. Adam Easton aliripoti kutoka mjini Warsaw akisema kuwa ajali hiyo ni pigo kubwa raia wa Poland.


Alisema kuwa Waziri Mkuu,Bw. Donald Tusk alibubujikwa na machozi wakati alipoelezwa kuhusu ajali hiyo.
Wazara ya majanga ya dharura,aliliambia Shirika la Habari nchini humo, Itar-Tass alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 5 kwa saa za Moscow.

Msemaji wa Wizara hiyo,Bi. Irina Andrianova alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mjini Moscow kwenda Smolensk lakini hakuna taarifa za watu waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Gavana wa Jimbo la Smolensk, Bw. Sergei Antufiev alikiambia kituo cha televisheni ya Urus kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyenusurika.
"Ilikuwa ikijiandaa kutua lakini ndege ya rais wa Poland haikuweza kufanya hivyo ,"alisema.


BBC Imetafsiliwa na WIILY MATIUS

No comments:

Post a Comment