header

nmb

nmb

Thursday, January 21, 2010

Mhandis wa bara bara Mkoani Mbeya apuuza agizo la Rais Kikwete.

mabasi ya abiria yakiwa yamekwama kwenye moja ya barabara mbovu Tanzania


source; Esther Macha, Mbozi

WANANCHI wa kata mbili za Kapeta na Kamsamba Wilayani Mbozi wamemtaka Mhandisi wa bara bara Mkoani Mbeya kutengeneza bara bara kama alivyopewa agizo na Rais Kikwete wakati wa ziara yake mwaka jana ,hali iliyopo hivi sasa kwa bara bara hiyo ni mbaya kiasi kwamba magari ya abiria yanakaa njiani kwa muda wa siku nne na kwamba hali hiyo inaweza kuhatarisha maisha ya wakazi wa kata hizo mbili .


Imeelezwa kuwa awali Rais Kikwete wakati wa ziara yake mwaka jana alitoa agizo kwa Mhandisi wa bara bara Mkoani hapa kutengeneza bara bara hiyo mara moja lakini agizo hilo halikufanyiwa kazi mpaka leo hii.


Akiihabarisha blog hii juzi Mwenyekiti wa kijiji cha Kamsamba , Bw. Vitus Kauzeni alisema ubovu huo wa bara bara umekuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa eneo hilo kwani imekuwa ni vigumu njia hiyo kupitika kirahisi hivyo inawalazimu magari yanayosafirisha abiria kukaa njiani kwa muda wa siku nne.

“Unajua ndugu mwandishi mwaka jana Rais alipokuja alitoa agizo kuwa bara bara hiyo itengenezwa mara moja kuanzia tarehe aliyokuja lakini kilichotushangaza bara bara hiyo baada ya siku tano ilianza kutengenezwa lakini kwa kuruzwa tu si ubora uliotakiwa hivyo mateso ya wananchi bado yapo pale pale hivyo bado tunahitaji marekebisho zaidi ili hii adha ya kulala njiani tuepuke nayo”alisema Mwenyekiti huyo.


Alisema kuwa licha ya kufanya matengenezo hayo lakini bado ubovu umebaki kwa kiwango kile kile na shida bado itaendelea kuwepo kama miaka mingine ,hii kwetu ni hatari kwani maisha yamekuwa ni magumu kwa kiasi kikubwa kwani muda mwingine bara bara hiyo maji yanajaa kiasi kwamba kunakuwa hakuna mawasiliano kabisa. Alibainishja kuwa tatizo la kujaa maji kwenye bara bara linatokana na na kutokuwa kwa mifereji hivyo tunaomba Rais apewe taarifa ya ubovu huu na Mhandisi aliyepewa majukumu na Rais ya kutengeneza afanye hivyo kama alivyoagizwa na Rais.


Aidha Bw. Kauzeni alisema kuwa anachoomba ni kwamba Rais Kikwete aweze kufikishiwa kumbu kumbu hizo kuwa wananchi wa Kamsamba na Tarafa nyingine ya Kapeta bado wanaendelea kupata shida ya tatizo la bara bara licha ya kutoa agizo.

No comments:

Post a Comment