header

nmb

nmb

Wednesday, January 27, 2010

KOVA ANAPO CHAPA KAZI VIBAKA WANAKOMA


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam lina washikilia wafanyabiashara wawili kwa kosa la kukutwa na bidhaa bandia aina ya Always zenye thamani ya sh 60,000,000.
Wafanyabiashara wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Bw. Paulo Lema kutoka mjini Arusha na Bw. Mazahel Meghji.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Bw. Suileman Kova alisema bidhaa hizo zikiwa katika magari manne tayari kwa kusafirishwa kwenda mikoani zilikamatwa jana katika eneo la jangwani.

Kamanda Kova alisema baada ya kukamata bidhaa hizo alijitokeza mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Mazahel Meghji
Alisema baada ya mahojiano, Bw.

Meghji na alikiri kuwa bidhaa hizo ni mali yake ambazo alinunua kutoka kwa Bw. Paulo Lema ambaye ni wakala wa bidhaa hizo katika mkoa wa Arusha.


Baada jeshi hilo kutuma askari wake kwenda katika mkoa wa Arusha lilifanikisha kumkamata Bw Lema na kukamata always nyingine 8110 zikiwa zimehifadhiwa katika ghala linalomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

Kamanda Kova alisema katika ukaguzi huo ulihusisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na Shirika la Viwango (TBS) na TSCAN kwa ajili ya uhakiki zaidi.
mwisho.
MAGARI manne yamekamatwa yakiwa na bidhaa bandiaPol

No comments:

Post a Comment