Kijana akifua nguo yake katika dimbwi la maji mchafu yaliyotuama bila kujali kuwa naweza kupatwa na magonjwa ya mlipuko kama alivyonaswa na kamera ya sufianimafoto, hivi karibuni eneo la Nyerere Square mjini Dodoma.
*WAKAZI WA KIJIJI CHA KIEGEI NACHINGWEA WALIA NA TABU YA MAJI
Mkazi wa Kijiji cha Kiegei Kata ya Kiegei Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, akichota maji katika katika kisimani kinachotegemewa na wanakijiji, ambapo maji katika kisima hicho hupatikana kwa tabu.
Kutokana na tatizo kubwa la upatikanaji wa maji hayo na kisima hicho kuwa na kina kirefu, tayari kinamama watatu wamevunjika miguu kwa kutumbukia katika kisima hicho, na wengine kutumbukiwa usiku wakati wakipita eneo hilo bila kujua shimo hilo.
Kutokana na hali hiyo wanawake wa kijiji hicho wamesema kuwa hali ya uchumi katika kijiji chao inazidi kuporomoka siku hadi siku, jambo ambalo wasema inachangiwa na tatizo hilo la maji, kwani wanawake wengi hutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya kazi ya kuzalisha.
*KUTANA NA VAILET MAMA WA WATOTO 2 ALIYEKIMBIWA NA BABA WA WATOTO WAKE KUTOKANA NA ULEMAVU
Mama Vailet Nyamanga (41) akiwa na Mtoto wake Rose Nyamanga (9) wakikatiza katikati ya mitaa ya Nkuhungu Wilaya ya Dodoma Mjini katika Mkoa wa Dodoma, hivi karibuni. Rose ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule msingi Nkuhugu, Mama huyu, Vailet, ambaye ni mremavu wa viungo mwenye urefu wa futi mbili, Anaishi kwa kutegemea msaada kutoka kwa wasambaliwema ambapo kwa siku anaweza kujipatia sh. 2000 hadi sh. 4000.
Na mwanawe Rose ndiye hasa msaada mkubwa kwa mama yake ambaye humuongoza pindi wanapokuwa barabarani katika safari zao za kutafuta riziki na pia ndiye humuhudumia mama yake kwa kumsafisha pindi anapokuwa amejisaidia na pia humlisha chakula na kumuogesha na kumvarisha nguo.
Rose alianza kumhudumia mama yaketangu akiwa na umri wa miaka (5).
Mama huyo hadi sasa ana watoto wawili Rose akiwa ni wapili kuzaliwa wa kwanza ni wa kiume ambaye ana umri wa miaka (19), anayeitwa Cristopher Nyamanga, ambapo watoto wote alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, lakini hadi sasa baba wa watoto hao hawajulikani walipo baada ya kumkimbia baada ya kumpa ujauzito. kwa hisani ya Na Mkubaru Blog
No comments:
Post a Comment