header

nmb

nmb

Wednesday, January 2, 2013

JK AZINDUA MATOKEO YA AWALI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

2012
 Bango likionesha idadi ya Watanzania wakati wa uzinduzi wa matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi  uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete  akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Idadi ya Watanzania kwa sasa ni 44,929,002. PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kikundi cha uhamasishaji kutoka wilayani Temeke, kikishangilia kwa furaha wakati wa uzinduzi huo.
 Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa hafla hiyo
 Rais Jakaya Kikwete (kulia), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) na  Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi wakicheka kwa furaha baada ya uzinduzi huo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Kamishina wa Sensa,  akipongezwa na  viongozi wa serikali kwa kufanikisha sensa hiyo
 Baadhi ya viongozi wa vyama na serikali wakiwa katika hafla hiyo

 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani akihutubia wakati wa hafla hiyo
 Sasa ni wakati wa kuimba utenzi wa kusifu sensa hiyo
 Wanahabari wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Traiphone Mweji, Adamu Gire, Chris Mfinanga na Antony Siame.
 Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakishangilia huku wakiwa na mabango  ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete.

 Rais Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa na viongozi wengine wa Serikali pamoja na watumishi wa Ofisi za Taifa za Takwimu za Tanzania Bara na visiwani wakati wa uzinduzi wa matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi  kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Rais Kikwete kwa kufanikisha sensa hiyo
Rais Jakaya Kikwete akiteta na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa hafla hiyo

No comments:

Post a Comment