header

nmb

nmb

Monday, January 28, 2013


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amenusurika katika ajali iliyotokea juzi katika eneo la Bwawani, mkoani Morogoro.

Mashuhuda wa tukio hilo, walisema kuwa gari la Lowassa lenye namba za usajili T 676 AWW, nusura likutane uso kwa uso na basi la Kampuni ya Moro Best na badala yake liligongwa ubavuni.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, chanzo cha ajali hiyo kilitokana na mabasi mawili yaliyokuwa yakifukuzana, likiwemo basi la Moro Best.

Ilielezwa kuwa, mabasi hayo yalipofika eneo la Bwawani, dereva wa Moro Best alitanua njia kutaka kulipita basi walilokuwa wakifukuzana nalo, ghafla alijikuta akikalibiana uso kwa uso na gari la Lowassa lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam.

“Dereva wa gari la Lowassa alipoona anakutana uso kwa uso na basi la Moro Best, kwa ujasiri mkubwa aliamua kuliingiza gari hilo katikati ya magari mengine na katika kufanya hivyo, akajikutana gari lake likigongwa ubavuni,” alisema shuhuda wa tukio hilo.

Lowassa ambaye muda wote alikuwa amepigwa na butwaa, alipoulizwa kama amepata majereha alisema hakuwa na jeraha lolote.

Hata hivyo, alisema mkono wa Mungu ni mkubwa kwani alishuhudia jinsi gari lake na basi la Moro Best yalivyotaka kugongana uso kwa uso na hajui nini kimenusuru.

“Nililiona basi la Moro likitukabili uso kwa uso na gari langu na wakati hali hiyo inataka kutokea, nikakumbuka maneno ya wimbo mmoja hivi yanayosema “Hivi vyote vinatoka wapi? Hii ni huruma tu”.

Pamoja na ajali hiyo, Lowassa aliendelea na safari yake. Alikuwa akitoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoan 

Cape Verde yafuzu wa robo fainali ya AFCON

Timu ya taifa ya Cape Verde
Cape Verde imeandikisha historia nyingine kwa kufuzu kwa robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika baada ya kuibanjua Angola kwa magoli mawili kwa moja.
Cape Verde ambayo inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza ilitoka nyuma ya kufungwa bao moja kwa bila na Angola na kuandikisha ushindi wao wa kwanza katika fainali hizo.
Cape imemaliza na alama tano sawa na Afrika Kusini lakini ikizidiwa na wingi wa magoli.
Mshambulizi wa ziada Heldon, ndiye aliyeifungia Cape Verde bao lake la ushindi kunako dakika ya tisini ya mechi hiyo.
Angole ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kunako dakika ya 36 baada ya mchezaji wa Cape Verde kujifunga mwenyewe.
Mashabiki wa Angola
lakini vijana hao wa cape Verde walisawazisha kunako dakika ya 81 kupitia kwa mshambuliaji wake Varel.
Morocco nayo imeyaaga mashindano hayo katika raundi ya makundi sawia na Angola ambayo ilizoa alama mbili na moja mtawalia.
Kinyume na ilivyokuwa katika mechi kati ya Afrika Kusini na Morocco ni mashambiki wachache sana walihudhuria mechi hiyo na ushindi wa Afrika Kusini katika mechi yao ya mwisho huenda ukachochea mashabiki zaidi kufika katika viwanja mbali mbali wakati wa mechi ya robo fainali.
Cape Verde sasa inajumuika na Afrika Kusini na Ivory Cost ambayo tayari zimejikatia tikiti ya robo fainali ya mashindano hayo, yanayoendekea nchini Afrika Kusini.
Wawakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, kesho inajitosa uwanjani kucheza mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Mali, mechi ambayo ni sharti washinde ili wafuzu kwa robo fainali ya mashindano h  

Afrika Kusini yasonga mbele

Kikosi cha Afrika Kusini
Afrika Kusini, wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, imefuzu kucheza hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya 2-2 na Morocco.
Kwa matokeo hayo Afrika Kusini inaongoza kundi A ikiwa na pointi 5 sawa na Cape Verde, lakini ikiizidi kwa wingi wa magoli.
Katika mchezo wa leo Morocco ndiyo iliyoanza kufunga katika dakika ya kumi ya mchezo, likitiwa kimiani na El Adoua.
Matokeo hayo yaliyodumu hadi mapumziko.
Huku Morocco ikiamini kuwa imeshinda, ilishtukia Afrika Kusini wanasawazisha katika dakika ya 71 kupitia kwa Mahlangu.
Morocco haikukata tamaa kusaka ushindi, na iliwezakutia kimiani goli la pili katika dakika ya 82, mfungaji akiwa Abdelilah Elhafidi.
Kocha wa Morocco
Furaha ya Morocco ilidumu kwa dakika nne tu, kwani katika dakika ya 86, Afrika Kusini kupitia kwa mshambuliaji wake Rantie, walisawazisha na kukata tikiti ya kucheza robo fainali.
Afrika Kusini na Cape Verde ndizo zilizofuzu katika kundi A kucheza hatua ya robo fainali.
Morocco yenye pointi 3 na Angola yenye pointi 1 kutoka kundi A, zimeiaga michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2013.
Kundi B kesho litakuwa linakamilisha michezo yake, kwa Ghana kumenyana na Niger, huku DR Congo ikipepetana na Mali.Mpaka sasa Ghana ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, ikifuatiwa na Mali pointi 3, DR Congo pointi 2 na Niger

Dua La Afrika Mashariki yasalia mikononi mwa DRC

Timun ya Taifa ya Soka na DRC
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo inajianda kwa mechi yao ya makundi ya michuaano ya kuwania kombe la mataia ya Afrika, dhidi ya Mali.
Timu hizo mbili ni sharti ishined mechi hiyo ya Kundi B, ili ifuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.
Endapo timu hizo mbili zitashona nguvu, Mali, huenda ikafuzu kwa robo fainali, ikiwa mechi nyingine ya Kundi hilo kati ya Niger, itamalizika huku timu hizo zikitoshana nguvu au Ghana ikiibuka na ushindi.
DRC, inashikilia nafasi ya tatu katika kundi hilo baada ya kutoka sare mechi zao mbili za kwanza.
Timu ya taifa ya Mali
Kocha wa Congo, Claude LeRoy, anasema kikosi chake kinakabiliwa na kibarua kigumu kuipiku Mali.
‘‘Ushindi pekee ndio utakaotuwezesha kufuzu kwa robo fainali’’ alisema LeRoy.
Ni timu hiyo ya Congo, pekee ndiyo iliyofuzu kwa fainali hizo mwaka huu, kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Hata hivyo makocha wa timu hizo mbili watakuwa na wachezaji wao wote katika mechi hiyo.
Kocha huyo wa Congo amesema amewahimiza wachezaji wake kucheza mchezo wa kushambuliaili kuimarisha nafasi yao.
Naye kocha wa Patrice Carteron, amesema nia yao kuu ni kutoka sare, ili kujihakikishia nafasi katka raundi ijayo na ni lazima tusahau, kipigo tulichopata dhidi ya Ghana na kuangazia mechi dhi 

KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHMAN KINANA AKAGUA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma ili kukagua ujenzi wa uwanja huo unaofanywa na kampuni ya ujenzi ya Howard Humphrey
4Katibu wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa Dk. Asha Rose Migiro , Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana wakielekea kwenye magari tayari kwa kukagua ujenzi wa uanjwa wa ndege wa Kigoma
5Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakikagua uwanja wa ndege wa Kigoma leo.
6Mafundi wa kampuni ya Howard Humphrey wakiendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma.
9 Meneja wa uwanja wa ndege wa Kigoma Injinia Clipia Tesha akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana wakati alipotembelea kukagua uwanja huo akiongozana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na kutoka kushoto ni Dk. Asha Rose Migiro Katibu wa Halmashauri kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi CCM na Martin Shigela Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM.11Cleopa Mpembeni Meneja mradi wa Ujenzi wa Uwanja huo kutoka kampuni ya Howard Humphrey akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati ujumbe huo ulipotembelea kukagua ujenzi wa uwanja huo leo
12Meneja wa uwanja wa ndege wa Kigoma Injinia Clipia Tesha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana kukagua ujenzi wa uwanja huo leo

No comments:

Post a Comment