header

nmb

nmb

Tuesday, October 19, 2010

WANAHABARI WATIMULIWA WASIMPE POLE SUPER COCH MZIRAY!!

MZIRAI KOCHA WA VIUNGO SIMBA.
Familia ya kocha wa saikolojia wa timu ya SIMBA SYLESAID MZIRAY imeshindwa kuthibitisha taarifa za baadhi ya vyombo vya habari zilizodai kuwa kocha huyo amefariki Dunia

Baada ya kutembelea nyumbani kwa kocha huyo maeneo ya TABATA MAGEGENI ili kujua ukweli wa taarifa hizo lakini ukweli ulishindwa kupatikana baada ya mke wa kocha huyo kutokuwa tayari kuongelea suala hilo

Mke huyo wa kocha MZIRAY alidiriki kuwafukuza waandishi wa habari wa huku akidai kuchoshwa na waandishi wa habari ambao kila mara wamekuwa wakifuatia ukweli wa habari hizo.

Kumekuwa na taarifa za utata juu ya afya ya kocha MZIRAY ambaye kwa takribani wiki moja ameshindwa kuiongoza timu yake ya Simba katika baadhi ya michezo ya ligi kuu Tanzania bara ukiwemo ule dhidi ya watani wao wa JADI YANGA uliopigwa katika uwanja wa CCM kirumba na SIMBA kuambulia kichapo cha bao moja kwa bila.Habari na Picha kwa hisani ya Jane John.

No comments:

Post a Comment