header

nmb

nmb

Monday, September 6, 2010

TENDWA AWA CHOMOLEA WAANDISHI ADAI WAENDE KWA WAHUSIKA!!

Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa leo amesema hana taarifa yoyote ya kutoa kuhusiana na pingamizi la CHADEMA dhidi ya mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa aliahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi bila kuhusisha Bunge kitu ambacho kinaenda kinyume na sheria ya Fedha za Uchaguzi. Bw. John Tendwa alikuwa ameahidi kutoa taarifa baada ya siku tano hata hivyo leo waandishi wa habari tulipo kwepokwenda ofisini kwake kwa ajili kujua hatma ya suala hilo alisema leo anamkutano mwingine na kuhusu pingamizi la CHADEMA tayari ameshavijibu vyama na pia taarifa ipo Tume ya Uchaguzi ya Taifa . Hivyo akashauri waende kwa vyama husika na kuwauliza "nendeni kwa wahusika mkawaulize mkiona mtu analia basi mjue mambo yake si mazuri lakini mkiona mtu anafurahia basi mjue mambo yake poa" Hata hivyo amesema atakuwa na mkutano mwingine baadae leo mchana huu hivyo tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata kuhusiana na suala hilo. zaidi tembelea fullshangwe.blog spot.com

No comments:

Post a Comment