Wakazi wa Arusha kumuona Mustafa Hassanali live
Ni mgeni rasmi katika Onyesho linalofanyika New Arusha Hotel
Visura 10 kuonesha mavazi yaliyooneshwa na Mustafa Hassanali nchini Cameroon February na Zanzibar Julai 2010.
Mwanzilishi na muandaaji wa jukwaa la wanawake wajasiriamali Tanzania (TWENDE ) na Jukwaa la kukuza vipaji vya wabunifu chipukizi Swahili Fashion Week, ambae pia ni mbunifu maarufu wa mavazi, Mustafa Hassanali amealikwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya mavazi yanayofanyika jijini Arusha kwa muda wa siku mbili tarehe 23 na 24 ya mwezi huu katika hoteli ya New Arusha.
Maonyesho hayo yameandaliwa na Maridadi. Maridadi ni kikundi kinachojumisha wanawake watatu kutoka mataifa tofauti ya Tanzania, Austarialia na Uholanzi ambao wanaishi nchini katika jiji la Aruha na kujishughulisha na masuala mbalimbali yanayohusiana na mendeleo ya mwanamke.
Akielezea lengo la kuandaa maonyesho hayo, mmoja wa wanawake hao, Lilian Bulengo amesema kuwa “dhumuni kuu la kuandaa tukio hili linalojulikana kwa jina la “Maridadi Women Show” ni kuwakutanisha pamoja wanawake kutoka maeneo tofauti ya Arusha na Moshi katika Fashion Show, maonyesho ya biashara pamoja na kupata fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali yanayowakabili wanawake katika maisha ya kila siku hapaTanzania ikiwemo suala la unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji, wanawake na kuondokana na utegemezi na masuala ya uchumi na biashara kwa ujumla”.
.
KAMA UMENOGEWA TEMBELEA MICHUZI JR IONE KWA UNDANI
No comments:
Post a Comment