header

nmb

nmb

Tuesday, September 21, 2010

HONGERA NDUGUYANGU ERIC SHIGONGO!!

Mwalimu wa Kimataifa wa somo la Ujasiriamali, Eric James Shigongo amesogeza elimu nyumbani kwako na kukupa mafundisho yenye hadhi ya Chuo Kikuu cha Mtaani.

Shigongo atazindua CD inayoitwa Street University (Chuo Kikuu cha Mtaani) hivi karibuni, lengo likiwa kuwawezesha watu mbalimbali kujifunza somo la Ujasiriamali.

Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Shigongo alisema kuwa ameamua kutoa CD hiyo ili kutoa fursa pana kwa wajasiriamali chipukizi kujifunza mbinu mbalimbali za kunufaika kibiashara.

“Ndani ya CD hiyo natoa elimu bora kabisa. Elimu ya kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wakubwa. Elimu ya kuwakomboa Watanzania katika mambo ya kiuchumi,” alisema Shigongo na kuongeza:

“Nahitaji kuzalisha mabilionea wengi kadiri inavyowezekana, kwahiyo Watanzania wenye kiu ya kutaka kuwa mabilionea, wanaweza kunufaika kupitia CD yangu.”

Shigongo aliendelea: “Watu wajiandae kuipata hivi karibuni. Itapatikana kwenye maduka ya Zizzou Fashions.”ZAIDI TEMBELEA BLOG YA burudan mwanzomwisho

No comments:

Post a Comment