header

nmb

nmb

Friday, August 27, 2010

TARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI>MWENYEKITI WA TASWA KUKUTANA NA WANA HABARI JIJINI!!

Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto kesho saa sita mchana katika ukumbi wa hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali baada ya kuingia madarakani. Mambo hayo yanatokana na vikao viwili vya Kamati ya Utendaji, cha kwanza kilifanyika Agosti 21 mwaka huu na cha pili kitafanyika leo Alhamisi ambacho pia kitakuwa na umuhimu mkubwa. Baadhi ya mambo atakayozungumzia ni kuhusu mikakati ya kuwasaidia waandishi wa habari za michezo kwenye mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu, kalenda ya matukio ya Taswa na tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka 2010. Ni matumaini yangu kuwa waandishi watajitokeza kwa wingi ili kuja kumsikiliza Mwenyekiti, ambaye ataambatana na viongozi wengine walioingia madarakani Agosti 15 mwaka huu. Ikumbukwe huu ni mkutano wa kwanza atakaoufanya Mwenyekiti tangu ashinde kwa kishindo katika uchaguzi uliokuwa wa kidemokrasia. Naomba kuwasilisha, nikitarajia utawajulisha waandishi wako wafike kwenye mkutano ili tukijenge chama chetu.

No comments:

Post a Comment