header

nmb

nmb

Thursday, August 12, 2010

MPISHI WA OSAMA AHUKUMIWA KUAFUNGWA 14!!!





MAHAKAMA ya Guantanamo Bay imemuhukumu kifungo cha miaka 14 jela mpishi na dereva wa zamani wa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda, Osama Bin Laden baada kukiri kumsaidia kiongozi huyo.
Mzaliwa wa Sudan Ibrahim, al-Qosi alihukumiwa kifungo hicho jana baada ya kukiri kula njama na kusaidia ugaidi.
Hata hivyo, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa huenda akatumikia kifungo chini ya hapo kutokana na kukiri kosa ingawa hukumu hiyo itaendelea kuwa siri kwa muda wa wiki kadhaa.
Chini ya mkataba huo, Qosi pia alikubali kufanya kazi kama mlinzi wa Bin Laden na kumsaidia kuepuka kukamatwa na majeshi ya Marekani.
Hukumu hiyo sasa kupitiwa na Pentagon.

No comments:

Post a Comment