header

nmb

nmb

Tuesday, August 31, 2010

MADENTI NAO NIWAMIAKA 9 AFA MAJI DAR!!

OMARY Mohamed (9), mwanafunzi wa darasa la tatu kutoka Shule ya Msingi Tandika Azimio, mkazi wa Tandika, amekufa baada ya kuzama maji wakati akiogolea mto Kizinga, Kivule wilaya ya Ilala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema tukio hilo limetokea jana saa 7 mchana Mto Mzinga.

Imedaiwa kuwa mwanafunzi huyo na mama yake, Amina Omary (30), mkazi wa Tandika, walikwenda Kivule kusalimia ndugu zao ambapo mtoto huyo alitoka na kwenda kuogelea na wenzake.

Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Amana na Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.

Wakati huo huo, wakazi 15 wa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kujibu mashitaka ya kukutwa wakiwa na banghi pamoja na pombe haramu ya gongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, amesema watuhumiwa hao walinaswa jana 5 asubuhi, Makabe, Mabibo, Manzese na Jangwani.

Baadhi ya watuhumiwa hao ni Blandina Mathias (46), Zawadi Abdalah (22), John Muhere (36), Mohamed Athuman (22) na wenzao.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Mwisho…!

No comments:

Post a Comment