Mwanamuziki nguli wa Zimbabwe Oliver Mutukudzi tayari yuko jukwaani kwenye Hoteli ya Movenpick akifanya mambo makubwa pamoja na wanamuziki wake, mashabiki wanamshangilia kupita kiasi kutokana na uwezo wake wa kuimba awapo jukwaani ni burudani tosha kwa mashabiki wake waliohudhuria katika onesho hili kutoka mataifa mbalimbali usku huu jijini Dar es salaam ambapo mashabiki tayari wamenyanyuka kwenye viti vyao hawatulii kutokana na burudani inayoporomoshwa na mwanamziki huyo gwiji kutoka Zimbabwe barani Africa.
Oliver Mutukudzi ni mwanamuziki maarufu sana katika Afrika, Marekani na ulaya hasa pale alipopata nafasi ya kkufanya mahojiano na kituo cha televisheni cha kimataifa cha CNN na amefanya ziara nyingi za kimuziki katika Bara la Ulaya, Marekani na Afrika kwa ujumla
No comments:
Post a Comment