header

nmb

nmb

Monday, August 16, 2010

HOFU YA MASHETANI OFISINI,MKUU WA WILAYA AKIMBIA OFISI KUOKOA ROHO YAKE!!





WATUMISHI wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gama, amekumbwa na kizaazaa cha aina yake baada ya kupokea wageni wasio wa kawaida wenye fimbo na Biblia.

Wageni hao watatu ambao walifika katika ofisi hizo huku kila mmoja akiwa na shida tofauti.

Wakizungumza na blog ya pr,baadhi ya watumishi ambao hawakupenda majina yao kutajwa katika blog hii wamedai kuwa mgeni mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Tunu Shaaban, mkazi wa Buguruni, alidai kuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni hivyo amefika katika ofisi hizo kuomba msaada wa sh. 30,000 kwa ajili ya matibabu.

Wakati mgeni huyo akilazimisha kupewa msaada huo, mgeni mwingine ambaye jina lake halikufahamika alikuwa aking'ang'ania kuingia ofisi za mkuu huyo kwa nia ya kuomba fedha.

Hata hivyo, wakati wageni hao wakiendelea na purukushani hizo, ghafla alitokea mgeni mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Mmbungu, mkazi wa Chanika, na kutaka kuingia ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kwa madai kuwa alikuwa akizungumza naye kwenye simu.

Akizungumza na blog hili, mkuu wa wilaya hiyo amesema baada ya mgeni Mmbungu kukorofishana naye kutokana na kumsumbua usiku kwenye simu akidai kuwa yeye ni mtu wa heshima kubwa, anadai kuwa viongozi wa sasa hawamheshimu ingawa mishahara yao inatokana na mapambano yake.

Amesema kuwa wakati anazungumza na mgeni huyo ghafla alibadili matamshi na kuanza kutoa kauli zisizoeleweka ambazo zilizua tafrani katika ofisi hizo.

Amesema mgeni huyo alikuwa akilazimisha kupewa sh. 200,000, kisha akatoa Biblia aliyokuwa ameifunika na kitambaa chenye bendera ya rangi Tanzania na Marekani.

Pia alikuwa na chupa ya plastiki iliyokuwa na maji na fimbo nyeusi pamoja na vitu vingine vyenye asili ya uganga, jambo lililosababisha mkuu huyo kuondoka na kwenda katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, William Lukuvi.

Gama amesema alilazimika kwenda katika ofisi hizo kwa ajili ya kuhitajika kuhudhuria kikao. Hata hivyo, amesema ulinzi zaidi unahitajika kwa wageni wanaofika kwa viongozi mbalimbali ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

No comments:

Post a Comment