Nairobi, Kenya
RAIS wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi ametakiwa kujiheshimu kwa kutotoa maneno ya kashfa dhidi ya Rais wa sasa Mwai Kibaki.
Kamati ya Usalama nchini humo imemtaka Moi kumuheshimu Rais Kibaki kwa kuwa ndiye aliyepo madarakani kwa sasa. Ni kutokana na wawili hao kuwa na mtazamo tofauti katika kampeni kuhusu katiba mpya.
Rais Kibaki kwa upande wake anataka wananchi wa Kenya kuupitisha muswada wa katiba mpya, huku Moi akiongoza kampeni ya kupinga katika hiyo.
Pamoja na hivyo, kamati iliyoundwa ya kujenga utaifa imesema, mzozo huo wa kibinafsi unaathiri kazi zake.
Kutokana na kuwepo kwa mvutano huo, baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini humo wamekuwa na wasiwasi wa kuzuka kwa machafuko mapya kama yale yaliyotokea katika kipindi cha uchaguzi 2007/08 ambapo zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha yao.
Jana Moi ambaye aliwahi kuwa rais wa Kenya kwa miaka 24 alisema, Kibaki hatakiwi kumshutumu kwa kupinga muswada huo kwa kuwa, hakutimiza ahadi yake ya kubadili katiba ndani ya siku 100, wakati alipoingia madarakani mwaka 2002.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kujenga Utaifa (NCIC), Mzalendo Kibunjia alimtaka Moi kumheshimu rais na kutoa wito kwa mahasimu hao wawili kujizuia kutoa matamshi ambayo yanaweza kusababisha mvutano katika kampeni za kura hiyo ya maoni.
Dalili mbaya ya kuwepo kwa machafuko yanayokisiwa kutokea imeelezwa kuanzia Juni mwaka huu ambapo watu wasiopungua sita waliuawa baada ya bomu la kurushwa kwa mkono kutupwa katika mkutano wa kampeni ya kupinga rasimu hiyo mjini Nairobi.
Kutokana na hali hiyo, wabunge watano walishitakiwa kwa kile kilichoeleza kutoa matamshi ya chuki wakati wa kampeni hizo na kwamba malalamiko hayo yalifikishwa kwa NCIC.
Ghasia nyingi za mwaka 2007/08 zilitokea wakati uhasama katika uchaguzi ulipozusha mizozo ya kugombea ardhi, hasa katika eneo la Bonde la Ufa, sehemu anayotoka Moi.
Moja ya kipengele katika rasimu ya katiba mpya, ni kuunda tume ya ardhi ambayo itataifisha ardhi iliyopatikana kwa njia zisizo halali wakati wa utawala wa Rais Moi.
FBI YAOMBWA MSAADA
Marekani yaomba FBI kuisaidia uvujaji siri Afghanistan
Marekani
OFISA Usalama wa Marekani Robert Gates ameitaka Shirika la Upelelezi (FBI), kusaidia kuchunguza uvujaji wa siri za kijeshi nchini Afghanistan.
Hiyo imetokana na jumla ya kurasa 90,000 za siri zinazohusu viya vya Afghanistan kuchapishwa na kuweka katika mtandao hivyo kufanya ulimwengu wote kusoma siri hizo ambazo kwa kawaida huwa ni mali ya jeshi tu.
Gates alisema, kuchapishwa kwa kurasa hizo na kuweka katika mtandao ni hatari kubwa kwa usalama wa wanajeshi waliopo nchini humo na mikakati yao kwa ujumla.
Alisema kuwa, ni vema ukafanyika uchunguzi wa hali ya juu ili kuweza kubaini muhusika aliyewezesha kupatikana kwa nyaraka hizo na kuchapishwa mtandaoni.
Mtandao wa Wikileaks website ambapo ndio uliochapisha nyaraka hizo umeeleza, nyaraka hizo zinahusu vita na kazi mbalimbali za wanajeshi nchini humo kuanzia mwaka 2004-09.
"Ni muhimu kwamba tuchunguze, tabia hii ya kuvuja kwa siri hizo ni tatizo kubwa kwa usalama wa Taifa.
"Kuendelea kuvuja kwa nyara hizi muhimu pia ni hatari kubwa kwa usalama wa majeshi yetu, ushirikiano wetu pamoja na rafiki zetu Waafghanistan. Pia inaweza kushusha hadhi yetu na uhusiano wetu duniani," alisema.
Gates aliongeza kuwa, aliongea na mkurugenzi wa FBI Robert Mueller juzi na kumtaka kutoa ushirikiano wake katika kuchunguza uvujaji huo wa siri za jeshi.

Miili ya waliokufa Kongo yasakwa
Kinshansa, Kongo
WAOKOAJI nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamesema, wapo katika hali ngumu ya kutafuta miili ya watu waliofariki dunia kutokana na boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye mwingiliano wa Mto Kongo kwenye eneo la Jimbo la Bandundu magharibi magharibi mwa nchi hiyo.
Katika ajali hiyo iliyotokea Jumatano iliyopita, inaelezwa kuwa zaidi ya watu 80 walifariki dunia ambapo boti hiyo ilikuwa imebeba watu ya uwezo wake.
Boti hiyo ambayo iliyokuwa na wafanyakazi na abiria zaidi ya 200, inaelezwa kuzama kwake kulitokana na boti hiyo kugonga kingo za mchanga au mwamba hivyo kuyumba na mwishowe kuzama katika mto huo.
Pia inaelezwa, sababu kubwa ni kutokana na boti hiyo kuwa na uzito uliopitiliza uwezo wa boto hiyo, hivyo kusababisha kuyumba na hatimaye kukosa mwelekeo na kuzama.
Baadhi ya watu waliokuwa katika boti hiyo walielezwa kuokolewa ambapo baadhi yao walijiokoa wenyewe kutokana na ujuzi wao wa kuogelea na kwamba idadi kamili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo haijaweza kufahamika. Wananchi wa Kongo wamekuwa wakitumia usafiri wa maji kutokana na nchi hiyo kutokuwa na miundombinu ya barabara, reli ya kutosha kwa miongo kadhaa sasa.
Kutokana na hali hiyo, ajali nyingi za boti kuzama majini zimekuwa zikitokea na kusababisha vifo vya watu wengi ambapo Novemba mwaka jana, takribani watu 73 walifariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama Ziwa Tanganyika katika jimbo hilihilo la Bandundu.
Ilielezwa kuwa boti hiyo ilikuwa imebeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu.
Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo alisema, ajali hiyo ni pigo kutokana na kugharimu maisha ya watu pamoja na malizao.
WFP kununua chakula Afrika
SHIRIKA la Chakula duniani (WFP) limesema linajitahidi kuongeza kiwango cha chakula kutoka barani Afrika.
Mkuu wa WFP Josette Sheeran alisema, wanajitahidi kuhakikisha kuwa nchi 16 kutoka Afrika zitafaidika kutokana na mpango huo.
Alisema, katika Bara la Afrika wakati uhaba wa chakula ukitokea, mashirika ya misaada ya kimataifa hupeleka chakula ambacho hununuliwa kutoka nchi za kigeni.
Alisema, WFP imeona kuwa hali hiyo ni kikwazo katika shirika hilo na kwamba, shirika hilo limedhamiria kuondokana na tatizo hilo.
Miongoni mwa nchi ambazo zimetajwa kuanzwa katika mpango huo ni Uganda.
Mkrugenzi wa WFP nchini Uganda Stanlake Samkange alisema, fedha nyingi zitatumika kununua vifaa vitakavyoliwezesha shirika hilo, kununua kiwango kikubwa zaidi mahindi na maharage.
Vifaa hivyo vitatumika kuhifadhi na kusafisha chakula hicho, ili kiweze kufikia kiwango cha kimataifa.
Mwaka jana WFP lilitumia dola za Marekani millioni 220 kutoka Afrika.
Wakulima kutoka Uganda, ni baadhi ya wale waliofaidika.
mwisho
No comments:
Post a Comment