
Hatimaye Mchezaji wa Hispania Iniesta amemaliza kazi katika dakika ya 116 kipindi ya nyongeza wakati alipofunga goli zuri kwenye mchezo wa
fainali kombe la dunia la FIFA kati ya Hispania na Uholanzi kwenye uwanja wa Soccercity jijini Johanesburg nchini Afrika Kusini.
Ulikuwa ni Mchezo wa ushindani na ufundi wa hali wa juu kwa kila timu ambapo kila mchezaji alionyesha uwezo wake katika kusaidia timu yake ya taifa lakini kila kitu kina

mwisho wake kwani kazi yote ilimalizwa na Iniesta na kumuweka wazi bingwa mpya wa michuano hiyo ya kombe la Dunia.
Lakini jambo zuri zaidi ni kwamba bingwa huyu mpya ni mpya wa kweli kwani hajawahi kuchukua kombe hilo toka lilipoanzioshwa, lakini pia wapinzani wao Uholanzi nao hawajawahi kuchukua komba hilo.
Mimi naweza kusema kuwa michuano hii imewakutanisha wapinzani ambao hawajawahi kuchukua kombe hilo ni dhahiri kwamba mambo yamebadilika kwani mashabiki wengi walikuwa wakizipa nafasi kubwa timu kongwe kama vile Brazil, Italia, Ujerumani ,Argentina na zingine nyingi, lakini mambo yamekuwa tofauti sana kwani imechukua ubingwa huo Hispania ambayo haikutarajiwa pamoja na kwamba ina kiwango kizuri cha mpira na ina ligi bora kabisa Dunial La Riga.0 maoni

No comments:
Post a Comment