header

nmb

nmb

Thursday, April 8, 2010

WASANII WAPANIA KUJENGA KIJIJI CHA MAKAZI YAO YA KUDUMU. KITAKUWA SEHEMU YA UTALII NCHINI.

Mwenyekiti wa SHIWATA .akizungumza na Baadhi ya wadau waliofika katika kikao cha kupanga mkakati huo

SHIRIKISHO LA W ASANII TANZANIA SHIWATA
P.O. BOX 25578 Dar es Salaam, Tel: 0754261331
WASANII WOTE,
W ANAMICHEZO, NA W ANAHABARl, DAR ES SALAAM, TANZANIA.
'Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIW ATA) ambalo limesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa limekubaliwa kujiunga na Kijiji katika Wilaya ya Kisarawe, mahali ambapo Wasanii wataweza kujijengea nyumba zao na kuweza kuishi pamoja kwa Ujamaa na kujitegemea.
SHIWA TA imeamua kutafuta nafasi hii ili kuwakomboa Wasanii ambao wengi wetu huwa na mwisho mbaya kwa kukosa hata mahali pa kuishi pamoja na kuhangaika miaka mingi na kazi za sanaa.
SHIWAT A pia imeangalia hali za baadhi ya Wanamichezo na Waandishi wa Habari Nchini na imegundua kwamba mwisho wao pia huwa mbaya kama wa Wasanii - hivyo imeamua kuwakaribisha Wanamichezo na Waandishi wa Habari kujiunga na SHIWATA ili tuweze kuishi pamoja katika Kijiji chetu.
SHIW A TA inaamini kwamba Umoja ni nguvu na kama wote tutaungana na kuishi pamoja kwa malengo ya kuendeleza Utamaduni na Michezo hap a nchini basi baada ya muda mfupi kutakuwa na mafanikio makubwa na tunaamini hata Serikali yetu tutaipunguzia kazi katika kufanikisha maendeleo hayo.
Wasanii lazima wawe na Kadi ya Uanachama wa SHIW A TA na wamelipia ma1imbikizo ya ada ya kila mwaka ambayo ni Shs. 5,000/= kila mwaka.
Wasanii walio na Kadi ya SHIWATA na waliolipa ada za mwaka (angalau Shs. 10,000/=) watalipa tena Shs. 10,000/= kama ada ya kujiunga na Kijiji. Hivyo kwa Mwanachama hai wa SHIWATA atatakiwa kulipa angalau Shs. 20,000/= ili aweze kupata eneo katika KijUi hiki.

3. Kwa Wanamichezo na Wanahabari ambao watapenda kujiunga na Kijiji hiki:-
Kwanza itabidi walipe Shs. 25,000/= za kujiunga na SHIWATA ambapo watapatiwa kadi ya Uanachama
Zoezi hili ni la mwezi mmoja kuanzia tare he 03/04/20 I 0 mpaka 03/05/2010 ambapo kila mmoja awe amelipa.
Malipo yote haya yafanywe kwa Mhasibu wa SHIWA TA ndugu Asha Salvador ambaye atatoa stakabadhi au yalipwe moja kwa moja katika Account ya SHIW AT A No. 010 00173760 katika Benki ya Akiba ya Posta Tanzal}ia.
-
Kila mwombaji wa kutaka kujiunga na Kijiji hiki ataleta picha mbili na atajaza fomu maalum kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi.
Ni matarajio yetu kwamba kila Msanii, Mwanamichezo na Mwanahabari popote alipo atafurahia mpango huu wa SHIW ATA ambao una malengo ya kuwaunganisha Wasanii wote, Wanamichezo na Wanahabari ili kuleta maendeleo katika nchi yetu.
Kutakuwa na Mkutano na Viongozi wote wa Vikundi, Vyama vya Sanaa, Michezo na Vyombo vya Habari, Filamu, Bendi za Muziki wa Dansi, Rap na Tarabu siku ya Jumatano tarehe 07/04/2010 saa 5:00 asubuhi katika ukumbi wa Chuo cha Splendid, llala Bungoni ambapo maelezo ya ziada yatatolewa. Viongozi wote mnaombwa kuhudhuria.

No comments:

Post a Comment