Mwana blog akipongezwa na Wenzake Rugen Kagaruki(alie kaa) na Machapta aliye simama wakati akionyesha cheti alicho tunukiwa leo na mkurugenzi wa Idara ya habari MAELEZO Mr Clement Mshana kwa niaba ya MEWATA Baada ya kuhudhulia mafunzo hayo
Kipeperushi cha Saratani kikionyesha piucha ya mmopja kati ya walioathirika na ugonjwa huo kwenye titi,Mgonjwa huyo alifariki. Akina mwenda na wenzake wamefundishwa jinsi ya kuwaibuwa wagonjwa kama hao majumbani
HABARI YENYEWE
WAANDISHI wa habari wa Kampuni ya Business Times inayochapisha magazeti ya Majira, Dar leo, Spotistarehe,Business Times na Maisha wametunikiwa vyeti vya kufuzu mafunzo ya ugonjwa wa Saratani.
Waliotunukiwa vyeti ni Bw.Peter Mwenda na Ally Suleiman ambao ni miongoni mwa waandishi wengine 20 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Akiwatunuku vyeti hivyo Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo Bw.Clement Mshana alisema kuwa waandishi hao ni mwanzo wa kujikita na kupata uelewa wa kuelimisha jamii juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
Bw.Mshana alisema kuwa kutunikiwa vyeti hivyo kutatoa changamoto kwa waandishi wengine kujifunza chanzo na dalili za ugonjwa huo ili kuutokomeza nchini ambao hivi sasa umekuwa tihio jamii hasa kwa akinamama.
Naye Daktari wa Afya ya Jamii, Dkt Ally Mzige alisemamafunzo hayo ni mwanzo wa MEWATA na chama chao kutoa mafunzo ya jinsi ya kuandika habari za afya kwa watanzania.
Dkt.Mjige katika mafunzo hayo waandashi walifundishwa dalili za saratani ya matiti kuwa ni kivimbe katika titi au kwapa, mabadiliko ya umbo na ukubwa wa titi, mabadiliko ya rangi ya ngozi ya titi na mabadiliko ya chuchu kwa kuingia ndani au kutoa maji maji ya rangi kama damu.
Alisema kuwa unaweza kujitambua au kugundua una tatizo la saratani kwa kutumia njia picha,kujitazama kwenye kioo na kujikagua sehemu mbalimbali wakati wa kuoga.
Katika hafla hiyo ambaye pia ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MEWATA, Dkt. Sarah Maongezi, Dkt. Alfred Katengile na Dkt.Maryrose Gattas waliokuwa wakifunzi wa mafunzo hayo walihudhuria..
No comments:
Post a Comment