header

nmb

nmb

Thursday, April 8, 2010

Mgombea Udiwani Pugu Kajiungeni kizimbani kwa ujambazi ,Makamba apagawa!!


Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba katika pozi tofauti

HABARI
KADA wa Chama cha Mapinduzi wa Kata ya Pugu Kajiungeni,Patrick Kumburu (30)amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kinondoni kwa tuhuma za mauaji ya kutumia silaha.

Mshakiwa huyo ambaye aliwahi kutangaza nia ya kugombea udiwani wa Kata ya Pugu Kajiungeni kupitia CCM alifikishwa jana mahakamani na wenzake sita.
Mwendesha Mashtaka, Bi. Munde Kalombola akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kinondoni Bw. Ferdinand Kiwonde mshtakiwa huyo anahusishwa na mauaji ya watu wawili Pascal William na Audax Peter kwa kuwapiga risasi eneo la Ubungo Darajani, Februari 21, mwaka huu.
Katika kesi hiyo washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kuvamia gari lililokuwa mbele yao likiwa katika foleni barabara ya Mandela eneo la Ubungo Darajani lilikiwa na abiria watatu wakiwemo watu wawili ambao ni marehemu na mtu mwingine Bibi Fitina Said (51)aliyenusurika wakidai wapewe fedha.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Peter Moyo, Frank Libanga, Peter Kitosi, Fesal Hozza na Waziri Mzee ambao kwa pamoja wamerudishwa rumande hadi Aprili 21, kesi yao itakapotajwa.

Mshakiwa huyo ambaye ni wa sita kati ya saba, alijisalimisha katika kuto cha Poliso Stakishari baada ya kutajwa kuhusika na matukio ya ujambazi na gari lake kukutwa na bunduki iliyotumika katika mauaji.

Mshtakiwa wa kwanza Geofrey Nyansio maarufu kwa jina la Jeff anashtakiwa kwa makosa mengine kumi ya wizi wa kutumia silaha katika matukio tofauti katika jiji la Dar es Salaam.

Jeff anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa kutumia silaha Februari 2009, Tangi Bovu baada ya kumtishia kwa bundiki Jenifa Elias na kupora mali zenye thamani ya sh. mil. 2.

Nyingine ni ya Machi 17, mwaka huu akiwa na wenzake alivamia duka la Bathelomeo Baganda na kuiba mali zenye thamani ya sh. mil. 11.3 na kutuhumiwa kuiba gari T213 ARX yenye thamani ya sh. mil. 9 baada ya kumtishia kwa bastola Bw. Paul Weseslaus hotelini.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu mashtaka hayo kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji. anaripoti kamanda Mwenda wa Email.mwendapeter5@yahoo.com

No comments:

Post a Comment