WAPENDWA wasomaji wa safu hii nyeti inayozungumzia mambo mbalimbali yahusiyo jamii, mapenzi na ndoa kwa lengo la kuelimishana, leo nipo tena nanyi katika kona hii kwa ajili ya kuendelea na kazi hiyo.
Katika mada yetu ya wiki iliyopita nilizungumzia matatizo yanayotokana na kuingilia uhuru wa wachumba na athari zake. Nina imani wasomaji wangu mlifurahia mada hiyo.
Katika mada yetu ya leo nitazungumzia dalili zinazoashiria kuvunjika kwa uchumba. Nawaletea mada hii kutokana na maswali niliyoulizwa na wasomaji wangu likiwemo hili la uchumba.
Kuna dalili zisizopendeza ambazo zikionekana katika uchumba inafaa uchumba huo ufe.
Lakini kama inavyoonekana katika maswali yaliyoulizwa, bado kuna vijana ambao wanashindwa kutambua dalili hizo.
Wengine hawajui utaratibu unaofaa kufuatwa kuvunja uchumba unaonekana hayumba.
Muulizaji alitaka kujua iwapo mchumba amelipa mahali baadaye akaanza kunigeuka kwa kuwa amempata mchumba mwingine, nifanye nini wakati wazazi wake walishatoa mahali?
Ili ni suala gumu lakini nitakujibu kwa ufasaha.
Kwanza usikubali kuoa mchumba ambaye ameanza kuonesha dalili za kutokukupenda.
Hata kama umemgharamia kiasi gani jambo kubwa linalotakiwa ni ninyi kujitahidi kwa kila njia ili mahali uliyotoa irudishwe.
Unaweza ukang'ang'ania kumuoa lakini baadaye ukajuta ni kwa nini ulifanya hivyo. Mchumba akianza kuonesha dalili hizo za kuwa na mwanaume mwingine huyu hafai.
Mwingine alitaka kujua iwapo mchumba ana tabia isiyofaa kuna haja ya kumuonya ili ajirekebishe au yafaa kuachana naye?
Jibu. Inategemea kasoro aliyonayo ni kubwa kiasi gani.
Kama ni jambo dogo ambalo umeligundua baada ya kuanza uchumba unaweza kumwambia jinsi unavyochukizwa na jambo hilo.
Kama atajirekebisha basi uchumba wenu unaweza kuendelea.
Utakuwa ukijidanganya kudhani kuwa mchumba wako anaweza kubadilika tabia yake baada ya ndoa. Ikishindikana wakati wa uchumba achana naye.
Hata kama kasoro hizo utazigundua muda wa kufunga ndoa utakapokuwa umekaribiana usikubali kuingia kwenye mkataba wa pingu za maisha na mwanamke ambaye hakufai.
Msomaji mwingine aliuliza kuwa anaye mchumba wa siku nyingi lakini siku hizi amebadilika.
Siku hizi ameanza kuwa na tabia mbaya japo nampenda, naomba ushauri nifanyeje?
Jibu: Nakushauri usianze kutafuta mwingine . Kufanya utakuwa unazidi kiharibu uhusiano wenu.
Jibu: Nakushauri usianze kutafuta mwingine . Kufanya utakuwa unazidi kiharibu uhusiano wenu.
Njia nzuri ni wewe kushauriana naye kwanza ili kutafuta muafaka. Endapo itashindikana kukubaliana ndipo unaweza kuchukua uamuzi wa kuvunja uhusiano wenu.
Inafaa zaidi ukimweleza sababu za kuvunja uhusiano wenu. Kwa vyovyote ni vizuri kuwashirikisha wazazi kwanza kabla ya kuvunja uchumba ambao ulishajulikana rasmi.
Baada ya uchumba kuvunjika jihadhari na maneno utakayohusu mchumba huyo. Wengi watataka kukuchota ni kwa nini mmeachana. Kamwe usishawishike kutoa siri zake au kumlaumu.
Ukifaulu kufanya hivyo utakuwa umejipatia sifa nzuri ya kupata mchumba.
Mwingine alitaka kujua kama ni vizuri kupokea zawadi za mchumba au hapana. Kulingana na mazingira au mila mbalimbali kuna zawadi maalum ambazo zinatambulikana katika kuposa mchumba.
Kwa kawaida zawadi hizo hurudishwa au kulipwa endapo uchumba utavunjika. Kwa hiyo ni vizuri kupokea zawadi kama hizo ili kuthibitisha makubaliano ya uchumba.
Pia si vibaya kuepana zawadi za upendo, lakini kuna mambo machache ya kujihadhari nayo. Kwanza si vizuri zawadi hizo ziwe za upande mmoja, yaani si vizuri mmoja awe tu ndiye anayetoa na mwingine awe ndiye tu anayepokea..
Wote wawili ni lazima wajitahidi kupeana zawadi. Zawadi za aina hii hazirudishwi hata kama uchumba utavunjik.
Yafaa kuwa mwangalifu wakati wa kutoa. zawadi na kujihadhari kupofushwa na hongo. Mchumba anaweza kukuonga zawadi nyingi akawa anatambua lkwamba upendo wenu ni vuguvugu. Kwa njia hiyo anadhani moyo wako utalainika.
Lazima ujihadhari sana ili usije ukampenda mchumba kwa sababu ya zawadi zake badala ya kumpenda kwa sababu ya jinsi yeye mwenyewe alivyo.
Wala usisite kumkataa mchumba ambaye ameanza kuonekana ana tabia mbaya eti kwa vile umeshapokea zawadi nyingi kutoka kwake. Kwa mawasiliano zaidi tumia barua pepe, gladnessmboma@yahoo.com. Pia Gazeti la Majira Jumapili
No comments:
Post a Comment