KAMANDA MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI M MPINGA AKIKABIDHI CHEWTI KWA MUHITIMU MRS.PATRICKCHUONIHAPO KOZI FUPI .
BAADHI YA WAHITIMU WAKIFUATILIA KWA MAKIMNI MAHAFARI HAYO YA PILI CHUONI HAPO
WAHITIMU HAO WAKIWA NA VYETI VYAO
MWENYE FUFAHA BAADA YA KUKABIDHIWA CHETI KWA NIABA YA WENZAKE WOTE
KAMANDA mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bw. Mohamed Mpinga amewataka wahitimu 304 wa mafunzo ya udereva kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kutii sheria wanapokuwa barabarani.
Akizungumza katika mahafali ya pili ya Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) katika fani ya udereva, usafi na mapambo Dar es Salaam jana Bw.
Bw. Mpinga alisema shule za udereva nchini ni 292 lakini kati ya hizo ni chache zinazotumia mtaala mpya wa sheria za barabarani uliozinduliwa mwaka 2009 ambao unawataka kufundisha sheria za matumizi ya barabara.
Alisema siku zijazo Serikali kupitia kikosi cha usalama barabarani inatarajia kuboresha hali ya usalama barabarani kwa kutoa leseni ambazo nakala zake zitaonekana kwenye komputa nchi nzima hivyo ili kudhibiti madereva feki.
Mkuu wa Chuo cha VETA, Bw. Samuel Ng'andu akisoma risala ya chuo alisema asilimia 80 ya ajali zinazotokea nchini zinatokana na makosa ya kibinadamu ambayo yanaweza kuzuilika.
Bw. Ng'andu alisema chuo hicho kinatambua mchango mkubwa kinachotoa kwa taifa kupitia mafunzo yenye ubora unaostahili na kuwa wadau muhimu katika sekta ya barabara.
Alisema VETA imekuwa ikitoa zaidi ya wahitimu 3,000 wa mafunzo ya udereva kwa mwaka na kutokana na wingi huo kimejipanga kujenga shule ya mafunzo ya udereva na usaili.
"Chuo kina nafasi kubwa ya kupunguza ajali barabarani kama madereva watapata nafasi ya fundishwa, wakafundishika na kuwapima uwezo wao kushirikiana nanyi trafiki kabla hawajapata leseni, naamini tutakuwa na madereva mahiri" alisema Bw. Ng'andu.
Alisema walimu wengi wanaotoa mafunzo ya udereva wamekuwa wakifanya kazi hiyo bila kupitia kozi fupi za ualimu wa madereva ili kutoa mafunzo na maboresho yaliyokamilika.
WAHITIMU HAO
KAMANDA MPINGA AKIONDOKA ENEO LA CHUO HICHO BAADA YA HUTUBA YAKE.KULIA ANAYE MSINDIKIZA NI MKUU WA CHUO HICHO SAMUEL NG'ANDU

HUTUBA HII
KAMANDA mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bw. Mohamed Mpinga amewataka wahitimu 304 wa mafunzo ya udereva kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kutii sheria wanapokuwa barabarani.
Akizungumza katika mahafali ya pili ya Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) katika fani ya udereva, usafi na mapambo Dar es Salaam jana Bw.
Mpinga alisema wahitimu hao watakapopata leseni wanatakiwa kufuata sheria inayowakataza kuendesha mwendo kasi,vyombo chakavu na wakiwa wamelewa.
Bw. Mpinga alisema shule za udereva nchini ni 292 lakini kati ya hizo ni chache zinazotumia mtaala mpya wa sheria za barabarani uliozinduliwa mwaka 2009 ambao unawataka kufundisha sheria za matumizi ya barabara.
Alisema siku zijazo Serikali kupitia kikosi cha usalama barabarani inatarajia kuboresha hali ya usalama barabarani kwa kutoa leseni ambazo nakala zake zitaonekana kwenye komputa nchi nzima hivyo ili kudhibiti madereva feki.
Mkuu wa Chuo cha VETA, Bw. Samuel Ng'andu akisoma risala ya chuo alisema asilimia 80 ya ajali zinazotokea nchini zinatokana na makosa ya kibinadamu ambayo yanaweza kuzuilika.
Bw. Ng'andu alisema chuo hicho kinatambua mchango mkubwa kinachotoa kwa taifa kupitia mafunzo yenye ubora unaostahili na kuwa wadau muhimu katika sekta ya barabara.
Alisema VETA imekuwa ikitoa zaidi ya wahitimu 3,000 wa mafunzo ya udereva kwa mwaka na kutokana na wingi huo kimejipanga kujenga shule ya mafunzo ya udereva na usaili.
"Chuo kina nafasi kubwa ya kupunguza ajali barabarani kama madereva watapata nafasi ya fundishwa, wakafundishika na kuwapima uwezo wao kushirikiana nanyi trafiki kabla hawajapata leseni, naamini tutakuwa na madereva mahiri" alisema Bw. Ng'andu.
Alisema walimu wengi wanaotoa mafunzo ya udereva wamekuwa wakifanya kazi hiyo bila kupitia kozi fupi za ualimu wa madereva ili kutoa mafunzo na maboresho yaliyokamilika.
KWA HISANI YA PETER MWENDA WA GAZETI LA MAJIRA
No comments:
Post a Comment