header

nmb

nmb

Sunday, March 21, 2010

TAARIFA KUTOKA POLISI KANDA MAALUM YA DSM.

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA DSM S.KOVA .

WATU wawili wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti akiwemo mlinzi wa Kampuni ya Panic Security System ya jijini Dar es Salaam kugongwa na gari la mafuta eneo la Sigara, barabara ya Nyerere na kufariki papo hapo.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke Bw.David Misime alisema katika tukio hilo barabara ya Nyerere eneo la Sigara gari T 381 AUK aina ya Fuso Tanker likitoka BP Kurasini kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) likiendeshwa na Bw.Mikidadi Hamisi (58) lilimgonga mlinzi Bw. Shaban Juma (25).


Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Temeke na dereva ameshikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi na kabla ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Bw. Misime alisema katika tukio la pili, mwendesha pikipiki Daudi Charles (35)aligongwa na gari T502 AWK iliyokuwa ikiendeshwa na Bw. Yusuph Moleli (33) saa moja jioni juzi katika eneo la Kibugumo barabara ya Feri.


Kamanda Misime alisema gari hilo lilikuwa linatoka Feri kwenda Kibugumo lilimgonga mwendesha pikipiki huyo aliyefariki papo hapo na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Vijibweni na masako unaendelea kumtafuta dereva.


Wakati huo huo nyumba ya daktari aliyefahamika kwa jina moja la Dkt. Mosha (48) iliyopo Kijitonyama Kisiwani Wilaya ya Kinondoni imeteketea kwa moto uliozuka ghafla na kuunguza vitu vyote vilikuwemo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Kionondoni Bw. Elias Kalinga alisema tukio hilo lilitokea jana, moto huo uliteketeza nyumba ya vyumba sita na mali zilizokuwemo, thamani na chanzo cha moto huo hakijajulikana.

No comments:

Post a Comment