MUNGU ZIWEKE ROHO ZA MAREHEM PEPONI. prhabari kwa wote Pia inaungana na Ndugu na jamaa wa Marehemu katika kipindi hiki kizito cha Msiba
ABIRIA zaidi ya 11 wamekufa papo hapo katika ajali mbaya ya barabarani baada ya lori la mafuta lenye tela kugonga na kuiburuza mtaroni kisha kukandamiza daladala aina ya kipanya katika barabara ya Morogoro eneo Kibamba, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi ya Dar es Salaam, Bw. Elias Kalinga akizungumza ilipotokea ajali hiyo eneo la Kwa Mangi, Kibamba jana alisema idadi kamili ya maiti waliokufa katika ajali hiyo huenda ikaongezeka baada ya miili ya marehemu hao kukatika vipande vipande.
"Mpaka sasa inadadi ya maiti ni 11 lakini idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu miili imekatwa katwa na kutenganishwa viongo vya mwili"alisema Kamanda Kalinga.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri wakati lori lililokuwa limebeba mafuta ya taa aina ya FIAT IVECO T186 ABP likiwa na tela T 192 ABP mali ya Kampuni ya Mahmod Mohamed Duale Transporter likitokea Dar es Salaam kwenda Isaka, Shinyanga kugonga Hiace iliyokuwa ikitoka Kongowe, Kibaha kwenda Ubungo Dar es Salaam.
Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa lori hilo lilivuka kutoka upande wake kwenda upande wa pili wa barabara na kugonga kipanya T615 AJW ambacho kukiburuza kwa umbali wa mita kadhaa kabla ya kukandamiza mtaroni kufanana na chapati.
Katika eneo la ajali, kazi ilikuwa ngumu iliyotumia takribani saa kumi kunasua miili ya watu waliokandamizwa na lori hilo kutokana na kutokuwa na vifaa vya kisasa vya kunyanyua uzito mkubwa.
Wakati wengine wakitafuta njia ya kunasua miili hiyo wakazi wengine wa eneo hilo walivamia eneo hilo wakiwa na ndoo za kuchota mafuta yalikuwa wanamwagika baada ya kutoa tenki la mafuta.
Askari wa jeshi la Polisi waliokuwepo kusaidia ulinzi, walifanya kazi ya ziada kuzuia watu kusogea eneo hilo hadi saa 7 mchana kazi ya kupakua mafua ilipofanyika na lori hilo kunyanyuliwa kunasua matiti waliokuwa wamekandamizwa.
"Tumezuia watu wasisogee eneo la ajali kwa sababu Walishatoboa tenki na kukinga mafuta,lakini matundu yamezibwa na limekuja tenki jingine kupakua mafuta ili uzito upungue winchi linyanyue lori hilo ili maiti wanasuliwe" alisema polisi mmoja ambaye hakutaja jina.
Katika jitihada za awali waokoaji, Kikosi cha Zimamoto cha Halamshauri ya Jiji la Dar es Salaam na wasamaria walifanikiwa kunasua maiti wawili ambao walipelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha.
Msemaji wa hospitali ya Tumbi, Bw. Gerald Chami alisema maiti mmoja imetambuliwa kuwa ni kondakta wa daladala hilo,Shukuru Mhagile (28) mkazi wa Kibamba CCM na msichana mmoja ambaye hajatambuliwa aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24-26.
Inadaiwa kuwa dereva wa lori la mafuta alikuwa amesinzia na gari hilo kuhama kutoka upande wake na kwenda kugonga kipanya hicho na kukandamiza watu waliokuwemo katika daladala hiyo.
Wananchi waliofurika eneo la tukio hilo walilalamkia Serikali kutokuwa na vifaa vya kisasa vya uokoaji na kusababisha kuchelewa kufika eneo la tukio.
"Hii kazi ya kunasua miili ya marehemu hawa ingeokoa maisha ya wale waliokuwa wamepata majeraha makubwa lakini walikuwa bado hai, ajali imetokea saa 11 alfajiri waokoaji wanakuja saa nne hata majeruhi watakuwa wamekufa" alisema mkazi mmoja ambaye alikataa kusema jina lake.
Kamanda Kalinga alisema atatoa taarifa nyingine ya ajali hiyo baadaye, maiti wamepelekwa hospitali ya Tumbi na wengine hospitali ya Mwananyamala kuhifadhiwa.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya CHADEMA, Bw. John Mnyika ametuma salamu za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki na wafiwa wote kufuatia ajali mbaya iliyotokea jana asubuhi Kibamba jijini Dar es Salaam.
Bw. Mnyika alisema CHADEMa inatoa mwito kwa Serikali na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vyanzo vya ajali za mara kwa mara katika eneo la Kibamba ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.
Alisema ikumbukwe kuwa Desemba mwaka 2007 ajali nyingine ilitokea eneo la hospitali ya Kibamba ikihusisha malori na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo mjamzito na wengine 11 kujeruhiwa.
Alisema Aprili mwaka 2008 bunge liliarifiwa kuwa jumla ya watu 181 wamepoteza maisha kwa kugongwa na magari kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2007 katika eneo la kuanzia Kibamba mpaka Ubungo kwenye mataa.
Alisema Mei 2009 madereva wawili walikufa baada ya magari yao kugongana uso kwa uso huko maeneo hayo hayo ya Kibamba na Januari 2010 watu 18 walijeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Morogoro eneo la Kibamba Darajani ambapo magari matano yaligongana kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment