header

nmb

nmb

Monday, February 22, 2010

BIRMINGHAM CITY FC





WANACHAMA NA MASHABIKI WAKIWA NA FURAHA

BIRMINGHAM City ni moja ya klabu ya chini England na yenye historia ndefu katika michuano mbalimbali nchini humo.

Klabu hii imeweka makazi yake katika jiji la Birmingham, England ambapo kwa mara ya kwanza haikuitwa Birmingham kama ilivyo sasa.

Ilikuwa mwaka 1875 ambapo kikundi cha vijana wa mji huo walikuwa wakijikusanya katika uwanja wa kituo kidogo cha afya, baada ya kusakata kandanda kwa miaka kadhaa huku wengine wakijiunga na kikundi hicho na wengine wakiamua kuacha, likatoka wazo kwa mmoja wa wanakikundi hicho cha soka kuanzisha timu kamili.

Lengo kuu likiwa ni kuweza kusaidiwa vifaa mbalimbali vya michezo kwa kuwa isingekuwa rahisi kwa kusaidiwa kama wasingefanya hivyo, kutokana na kuchezea katika uwanja wa kituo hicho cha afya, waliamua kuiita timu yao kwa jina la Small Heath F.C. mwaka 1888, ilikuwa ni baada ya miaka 13 bila jina.

Timu hiyo ilianza kupata wadhamini wa viwanda vidogo vidogo na matajiri wachache wapenda soka, hata wale wasiokuwa na uwezo lakini kutokana na mapenzi ya soka, waliamua kujitutumua na kupeleka michango yao.

Ilionekana kuwa timu hiyo imeanza kukomaa na kwa kuwa katika jiji hilo hakukuwa na timu kubwa, baadhi ya matajiri waliamua kuiboresha timu hiyo na ndipo walipoibadilisha jina na kuiita Birmingham FC mwaka 1905.

Kana kwamba haikutosha, timu hiyo ilizidi kuchakaza timu zingine katika jiji hilo, baada ya kuanzisha michuano mbalimbali ya majiji na miji tofauti, Birmingham FC ilichaguliwa kuwa mwakilishi wa jiji hilo na wakati huo ndipo ilipachikwa jina la Birmingham City mwaka 1943 .

Katika historia ya klabu hii, miaka iliyokuwa na mafanikio makubwa ni kuanzia 1950 hadi 1960 ambapo mwaka 1956 ilifika katika fainali za kombe la FA, pamoja na michuano ya Inter-Cities Fairs Cup mwaka 1960 na 1961 na kushinda.

Ni kipindi ambacho klabu hiyo ilitesa Englandi kuliko miaka yote mpaka sasa, ilikuwa ni kipindi ambacho kila mchezaji wa England alipenda kuchezea klabu hiyo ambapo ilikuwa ni miongoni mwa nafasi za juu 'big four'.

Kwa mara ya kwanza meneja wa klabu hiyo Leslie Knighton mwaka 1931 aliiwezesha klabu hiyo kufika katika fainali za FA Cup ambapo walipoteza mechi hiyo kwa ufungwa bao 2–1 dhidi ya West Bromwich Albion.

Lakini pamoja na kupoteza mechi hiyo, bado kwa misimu 18 mfululizo ilikuwa ikionekana kutesa katika michuano hiyo, hata hivyo kuzuka kwa vita vya pili vya dunia kulionekana kuiiathiri kwa kiwango kikubwa klabu hiyo.

Moja ya mambo yaliyo historia katika klabu hiyo ni mechi yake na Manchester City mwaka 1956, ni siku huzungumzwa na wapenzi wa klabu hiyo kwa miaka hiyo kutokana na kilichotokea uwanjani.


Ni mwaka ambao kipa wa Birmingham alitenguka mshipa mmoja wa shingo katika mechi hiyo ambayo Man City iliitungua Birmingham 3–1, Kipa huyo Bert Trautmann licha ya kuingia dakika 20 za mwisho za kipindi cha pili, alijikuta akibebwa kutolewa nje kutokana na adha ya mechi hiyo ambapo shuti moja lilimmaliza kabisa.
Katika msimu wa 1984/85, ni wakati ambao kwa mara ya kwanza ilikumbwa na misukosuko hatimaye kushuka daraja na kuwa daraja la pili, baada ya kushuka daraja, baadhi ya viongozi wa juu wa klabu hiyo wakatimua na kuiacha klabu ikiwa inaweweseka katika kila idara.

Ilikuwa Aprili 1989 klabu hiyo ilipigwa mnada ambapo wamiliki wawili ndugu wa kiwanda cha nguo waliojulikana kama Kumar Brothers nchini humo waliamua kununua timu hiyo.

Kutokana na utajiri wa wamiliki hao, taratibu klabu hiyo ilianza kunyanyuka ingawa bado matatizo yalikuwa yakijitokeza mara kwa mara.

Birmingham City kama klabu zingine, mara nyingi huweka mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa inashika kasi, tamaa ya kuonekana klabu bora ni kama ilivyo kwa klabu zingine zote.

Msimu wa 2003/04 kutokana na hali mbaya ya kiuchumi katika klabu hiyo, iliomba mkopo kwa tajiri aliyejulikana kwa jina la Mikael Forssell na kuifanya klabu hiyo kuanza kujipanga upya katika michuano mbalimbali nchini humo.
Usajili wa nguvu ulifanyika na kuanza kuipa uhai klabu hiyo, baada ya miezi miwili, timu hiyo ilikabidhiwa kwa mwenyekiti mpya David Gold ambaye mara baada ya kuingia alisema " sasa mabadiliko lazima yawepo, lazima tuingie katika nne bora na ikiwezekana tuwe namba tatu katika nne hizo."
Pamoja na hivyo, kutokana na kutokuwa na mipango madhubuti, ukata katika klabu, mambo hayo hayakuweza kufanikiwa ambapo hata katika mechi ya kwanza walipomenyana na Liverpool, walifungwa 7-0 katika michuano ya FA.


Kitu hicho kilisababisha klabu hiyo kuendelea kumong'onyoka kutokana na baadhi ya wachezaji wakali kuamua kukacha klabu hiyo.

Julai 2007, mfanyabiashara raia wa China katika jiji la Hong Kong Carson Yeung alijitokeza kununua hisa kwa asilimia 29.9 na kuifanya klabu hiyo kuanza kuwa na uhai upya.

No comments:

Post a Comment